Alhamisi, 7 Julai 2022

BALOZI KATTANGA ATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA KWENYE MAONESHO YA 46 YA KIMATAIFA YA SABASABA

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga amefanya ziara na kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam na kushuhudia huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa na Mahakama kwa wananchi, jana tarehe 6 Julai, 2022. 

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga akitia sahihi kwenye kitabu cha wageni wakati huo akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Kumbukumbu za Utawala Mahakama ya Tanzania, Bw. Daniel Msangi (kushoto) alipowasili kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam, jana tarehe 6 Julai, 2022.


 
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga (mwenye kaunda suti ya bluu) alipowasili kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam, jana tarehe 6 Julai, 2022.


Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga akipokea zawadi ya vitabu na machapisho mbalimbali kutoka kwa Muhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Dkt. Kevin Mandopi alipowasili kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga akipewa maelezo kutoka Kiongozi wa Kituo cha Huduma Kwa Mteja cha Mahakama, Bi. Evetha Mboya (aliyenyoosha mikono) ya namna kituo hicho kinavyotoa huduma zake kwenye katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga (aliyenyoosha kidole) akitoa maelekezo kwa mtoa huduma (hayupo pichani) wakati alipotemebelea Banda hilo.

(PICHA na Innocent Kansha - Mahakama)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni