Mhe. Balozi Charles Sanga akiwasilisha mada ya Uzalendo kwa washiriki wa Mafunzo elekezi yanayoendelea kufanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto. Amewataka kuwa Wazalendo na kuzingatia sheria na kanuni za kazi.
Mwanasaikolojia nguli, Bi. Sadaka Gandi akisisitiza jambo kwa Makatibu Mahususi alipokuwa akitoa mada ya jinsi
ya kukabiliana na msongo wa mawazo (Stress Management). Amewataka washiriki hao kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yako kwa kutokufanya kazi kwa hisia pamoja na kubadili mitazamo.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick
akiwasilisha mada kwa Makatibu Mahsusi kuhusu Maadili na Stahiki
mbalimbali kwa Wutumishi wa Umma katika mafunzo elekezi yanayoendelea katika
kutolewa katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Japhet Manyama akiwapitisha washiriki katika mada ya Tamaduni za
kimahakama kwenye mafunzo yanayoendelea Chuoni IJA-Lushoto.
Afisa Tehama Mwandamizi, Bw.
Allan Machella akiwafafanulia washiriki juu ya matumizi
sahihi ya mitandao ya kijamii na kuwaasa kutotumia mitandao hiyo kutoa
taarifa za Ofisi. Aidha, ametoa picha ya mifumo na hatua mbalimbali zinazochukuliwa kuelekea Mahakama Mtandao 'e-Judiciary'.
Bw. Hassan Kilenza, Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akiwasilisha mada ya Maadili na Mienendo ya Utumishi wa Umma kwa washiriki wa mafunzo elekezi yanayoendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakam Lushoto.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Sekela Mwaiseje akitoa Mada kwa Waajiriwa wapya wa Mahakama (hawapo katika picha).
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia Mada inayotolewa na Mwezeshaji (hayupo katika picha).
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Ufuatiliaji, Mahakama ya Tanzania, Bw. Sebastian Lacha akitoa mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Washiriki wa mafunzo elekezi yanayotolewa kwa Waajiriwa wapya wa Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni