Na Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama
Jaji
Mkuu na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Prof. Ibrahim Hamis
Juma amewataka wananchi kuhakikisha wanafanya juhudi binafsi kuzifahamu haki zao za msingi kabla ya kutafuta msaada wa kisheria.
Jaji
Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 22 Januari, 2023 jijini Dodoma katika hafla ya
uzinduzi wa Wiki ya Sheria iliyozinduliwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango baada ya kumalizika kwa matembezi
yaliyoanzia kwenye kituo Jumuishi cha Utoaji haki Dodoma na kuishia kwenye
viwanja vya Nyerere Square jijini humo.
Alisema
wananchi wanaotaka kutafuta haki, hatua ya mwanzo kabisa ni kuhakikisha
wanafahamu wao wenyewe haki zao kwa kusoma au kutafuta elimu ya kuwawezesha
kujua shughuli wanazofanya zinaongozwa na sheria ipi, kanuni na utaratibu upi”,
alisema Jaji Mkuu.
‘Wananchi
wakiwa kwenye ufahamu huo watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupigania haki
zao na kupata haki hiyo kwa urahisi”, alisema Jaji Mkuu.
Akifafanua
kuhusu kauli mbiu ya Wiki ya Sheria kwa mwaka huu, Jaji Mkuu alisema inahimiza
migogoro kumalizika haraka kwa njia ya usuluhishi. Alisema kuwa usuluhishi
utawezekana pale tu ambapo Mahakama, wadau pamoja na wananchi wataona faida za
kutumia njia hiyo katika kutatua migogoro.
“Katiba
ya nchi inahimiza usuluhishi, inaitaka Mahakama inaposikiliza mashauri ya jinai
Pamoja na yale ya madai ikuze na kuendeleza usuluhishi kwenye migogoro”. Alisema
Jaji Mkuu.
Alisema
utatuzi wa migogoro kwa kutumia njia ya usuluhishi una faida nyingi ambayo ni pamoja na kutatua migogoro kwa muda
mfupi na pia kwa gharama nafuu.
Kuhusu
matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli za
Mahakama, Jaji Mkuu amewataka wananchi kutokubali kuachwa nyuma katika matumizi
hayo kwani wakiachwa nyuma watapoteza ule ushindani na hivyo kushindwa na wengine.
Maonesho ya Wiki ya Sheria yanafanyika jijini katika viwanja vya
Nyerere Square jijini Dodoma kuanzia leo na yatamalizika Januari 29, 2023.
Aidha Siku ya Sheria nchini itakayofanyika tarehe 01 Februari, 2023 ambapo mgeni
rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo ni Msimamizi wa shughuli za Mahakama ya Tanzania ni miongoni mwa Taasisi wadau wa utoaji haki nchini zinazoshiriki kwenye Maonesho hayo. Baadhi ya taasisi nyingine zinazoshiriki kwenye maonesho hayo ni Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Wizara ya Katiba na Sheria, Tume ya Kurekebisha Sheria na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Jaji
Mkuu na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Prof. Ibrahim Hamis
Juma akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria leo tarehe 22 Januari, 2023 jijini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni