TAARIFA
KWA UMMA.
02 Januari, 2023 Dar Es Salaam
Mhe.
Prof. Ibrahim Hamis Juma,
Jaji Mkuu wa Tanzania, anasikitika kutangaza
kifo cha Mhe. Dkt. John Harold Kulimba
Utamwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa kilichotokea
leo tarehe 02/01/2023 katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa
anapatiwa matibabu.
Marehemu Mhe. Jaji Dkt. Utamwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la Damu ambapo tarehe 17 Desemba, 2022 alilazwa katika
Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Mnamo tarehe 18 Desemba, 2022 alihamishiwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili kuendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomfika.
Marehemu
Jaji Dkt. Utamwa
alijiunga na Mahakama ya Tanzania
tarehe 17/02/1992 akianzia ngazi
Hakimu Mkazi. Alipanda ngazi mbali mbali ndani ya Mahakama na hatimaye
aliteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 24/6/2010. Akiwa Jaji wa Mahakama Kuu
ya Tanzania, Marehemu Jaji
Dkt. Utamwa alifanya kazi katika kanda za Dar es
Salaam, Tabora, Mbeya na Iringa.
Kufuatia
Msiba huo, taratibu za maziko zinafanyika nyumbani kwa marehemu Madale jijini
Dar es salaam. Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kutolewa.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA
LA BWANA LIHIMIDIWE.
Imetolewa na
/Artemony Vincent Tiganya
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano – MAHAKAMA YA TANZANIA
Mhe Dkt. John Harold Kulimba Utamwa enzi ya Uhai wake
Mhe Dkt. John Harold Kulimba Utamwa enzi ya Uhai wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni