Na Waandishi wetu, Mahakama ya Tanzania
Mahakama
nchini jana tarehe 22 Januari, 2023 ilianza Maadhimisho ya Wiki ya Sheria
huku Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizindua wiki hiyo ya utoaji elimu ya
sheria kwa ngazi ya Makao Makuu jijini Dodoma.
Kwa upande wa Morogoro, Mwandishi wetu Evelina Odemba anaripoti kuwa, hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria kwa Mkoa huo ilizinduliwa kwa matembezi maalum yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Mwassa ambaye ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa uboreshaji mkubwa wa huduma zake.
'Mimi ni miongoni mwa waliokuwa wanatambua kwamba Mahakama ni chombo kilichojikita kwenye kuamua na kutoa hukumu pekee, lakini leo tumejua kwamba mtazamo huo ni potofu, hongera kwa Uongozi wa Mahakamakwa uboreshaji mkubwa wa kisera, kimtazamo na utendaji wa kazi kwani matokeo makubwa ya mageuzi yanayoonekana nchi nzima," alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Naye, Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Morogoro, Mhe. Paul Ngwembe ametoa rai kwa Watumishi na Wadau wa Mahakama kutoa elimu ya usuluhishi kwa wananchi bila kuwatoza gharama yoyote.
Yafuatayo ni matukio katika picha ya hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria katika Mkoa huo;
Jaji Mfawidi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, Mhe. Paul Ngwembe akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa wiki ya Sheria Kanda ya Morogoro.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama, Viongozi na wadau wakiandamana kutoka Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Morogoro kuelekea viwanja vya Kiwanja cha Ndege mkoani humo ambapo hafla ya uzinduzi ilifanyikia.
Afisa Tehama wa Mahakama-Morogoro, Bw. Tamimu Hussein akimuonesha Mgeni rasmi, Mhe. Fatma Mwassa (mwenye kitambaa cha damu ya mzee) namna ambavyo Mahakama imejiboresha kwa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Morogoro, Mhe. Gabriel Malata, kulia kwake ni Mtendaji wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Morogoro, Bw. Ahmed Ng’eni na kusoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Naibu Msajili wa Kituo hicho, Mhe. Augustina Mbando.
. Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza maandamano ya uzinduzi wa wiki ya sheria kuelekea Kiwanja cha Ndege ambako ndiko hafla ya uzinduzi wa wiki ya sheria ilipofanyikia.
Kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, mwandishi wetu Mayanga Someke anaripoti kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda
ya Sumbawanga, Mhe. Dunstan Ndunguru amewasihi wananchi
kutumia fursa ya wiki ya Sheria nchini kupata elimu ya sheria itakayotolewa na Watumishi wa Mahakama na Wadau wake.
“Kauli mbiu ya mwaka huu hii inabeba tafakari kubwa juu ya wajibu wa Mahakama na Wadau
katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu. Utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni kichocheo kikubwa cha
kukuza na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii na Taifa kwa ujumla kwa kuwa
usuluhishi huokoa muda na gharama kwa wadaawa na kwa Mahakama na hivyo kuwezesha
wadaawa kutumia muda na gharama inayookolewa katika shughuli nyingine za
kiuchumi," alisema Mhe. Ndunguru.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Sebastian Waryuba amesema ni jambo la kupongeza kuona kuwa katika kindi cha zaidi ya miaka 100 ya Mahakama ya Tanzania, Mahakama imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Mihimili mingine katika ujenzi wa Nchi yetu kwa kuzingatia sera ya uchumi endelevu, ushirikiano huo ni lazima uendeleze katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi.
"Katika maadhimisho haya ya wiki ya sheria nchini ni vizuri kutafakari kwa kina mambo yanayotakiwa kuboreshwa katika safari hii ya kukuza uchumi endelevu,miongoni mwa mambo ya kutafakari ni Pamoja na maadili ya baadhi ya watendaji wa Mahakam na vitendo vya rushwa ambavyo bado vinalalamikiwa na wananchi," alisema Mhe. Waryuba.
Matukio katika Picha uzinduzi wa Wiki ya Sheria kwa upande wa Mahakama Kuu-Kanda ya Sumbawanga
Kwa upande wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Mwandishi wetu, Ahmed Mbilinyi anaripoti kuwa, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Imakulata Banzi aliongoza uzinduzi wa maadhimisho wa wiki ya sheria, uzinduzi huo ulianza kwa matembezi maalumu yalioanzia katika viwanja vya Mahakama Kuu Bukoba na kuishia viwanja vya Mayunga Manispaa ya Bukoba.
Maandamano hayo baada ya
kuwasili viwanja vya Mayunga yalipokelewa na Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila ambapo alipata nafasi ya kusalimia pamoja na kutoa hotuba
fupi.
Katika hotuba yake, Mhe. Chalamila ameipongeza Mahakama kwa kuwaelimisha wadau wa Mahakama juu ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ambayo kwa kiasi kikubwa njia hiyo inapunguza gharama za uendeshaji mashauri, kupunguza kwa mlundikano wa mashauri Mahakamani, muda pamoja na kuwaacha wadau katika maelewano mazuri.
Katika
maonesho ya Wiki ya Sheria katika Kanda hiyo, elimu itatolewa na Majaji, Naibu Wasajili, Mahakimu pamoja
na Wadau wa Mahakama, wakiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya
Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Polisi, Magereza,Uhamiaji
na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe Albert Chalamila (mwenye 'scarf') akiwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe Immaculata Banzi (kulia kwa Mkuu wa Mkoa), Viongozi wengine wa Mahakama pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera mara baada ya kupokea maandamano ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria kwa mwaka 2023 katika viwanja vya Mayunga Manispaa ya Bukoba Mjini.
'Brass Band' pamoja na Timu ya Skauti wakiwa katika maandamano ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria kwa mwaka 2023.
Naye Mwandishi wetu kutoka Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Angel Meela anaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela amewahimiza wananchi kutatua migogoro mbalimbali kwa njia ya usuluhishi badala ya kukimbilia mahakamani.
"Utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi unaweza kusaidia wananchi wengi kwa kuwa utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala itapunhuza gharama na kuleta amani na hata mgogoro unapoisha hautaacha makovu," alisema Mhe. Mongela.
Pamoja na hayo Mh. Mongela ametoa wito kwa Mahakama juu ya utoaji elimu juu ya maswala ya kisheria na usuluhishi wa migogoro mbalimbali katika jamii kutumia elimu hii vizuri kwakuwa itawasaidia kupata muda mzuri zaidi wa kujishughulisha na shughuli nyingine za maendeleo badala ya kuwa kwenye migogoro na kesi mahakamani.
Sambamba na hayo naye, Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Mhe. Judith Kamala amesema katika maadhimisho ya wiki ya sheria
miongoni mwa shughuli zitakazofanywa ni pamoja na utoaji wa elimu na msaada wa
kisheria katika viwanja vya TBA , kutoa elimu katika shule mbalimbali za
sekondari, gerezani na kwenye vituo vya redio.
N Naye Catherine Francis wa Mahakama Kuu- Kanda ya Songea anaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Kanali Laban Thomas amewapongeza Viongozi na Watumishi wa Kanda hiyo kwa utoaji elimu ya sheria kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanaoufanya kwa kupitia njia mbalimbali kama redio na mihadhara mbalimbali.
K Alisema kuwa, mafanikio haya yametokana na
uongozi imara wa Mahakama Kanda ya Songea, hivyo amewaomba Wadau wote wa
Mahakama kuendelea kushirikiana zaidi na Mahakama ili kuweza kuendelea kukuza
uchumi wa nchi kwa kuendelea kuwaelimisha Wananchi juu ya mambo mbalimbali
yanayohusu sheria kwani kwa kutumia elimu hiyo wataweza kuleta mwamko kwenye jamii
kuweza kushirikiana na Serikali ili kupunguza matukio ya uhalifu.
P Kadhalika, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, amesema kwa sasa dunia ipo kwenye Mapinduzi ya viwanda hivyo kunahitajika kuwepo na utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi kwa kuwa ndiyo namna bora ya kutatua migogoro. Aliendelea kuzungumza kwa kuelezea umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kuwa pamoja na kupunguza muda wa usikilizaji wa shauri pia ni njia pekee ambayo ikitumika vizuri inatunza faragha za Wadaawa wote wawili na pia njia ya usuluhishi inaendeleza mahusiano mazuri baina ya pande zote mbili.
.
Baadhi
ya Watumishi na Wadau wa Mahakama wakiwa kwenye matembezi ya uzinduzi wa Wiki
ya Sheria nchini mkoa wa Ruvuma tarehe 22 Januari, 2023.
Mhe. Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Kanali Laban Thomas akizungumza na Wananchi, Wadau pamoja na Watumishi wa Mahakama Songea waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria, 2023.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kanda ya Songea, Mhe. Yose Mlyambina akizungumza
na Wananchi, Wadau pamoja na Watumishi wa Mahakama Songea waliohudhuria sherehe
ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria.
Kwaya
ya Watumishi wa Mahakama wakiimba wimbo maalumu wa uzinduzi.
Baadhi ya Wadau wa Mahakama (Jeshi la Uhamiaji) waliohudhuria sherehe ya uzinduzi.
Naye Mohamed Kimungu, Mwandishi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe anaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ameongoza matembezi ya watumishi,Wadau pamoja na wananchi katika matembezi maalumu ya uzinduzi wa wiki ya sheria nchini.
iri Mhe. kindamba amewataka wananchi kutembelea mabanda yaliyopo ili waweze kupata elimu inayotolewa katika mabanda hayo,Aidha amekemea ukatili wa kijinsia kwa watoto ulioshamiri (kulawati watoto wadogo) na kueleza ni jukumu la kila mmoja hasa vyombo vinavyosimamia haki na sheria kukemea na kuwachukulia hatua wale wote wanaobainikia kutenda makosa hayo.
M Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi-Songwe, Mhe Hassan Makube amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali mwaliko na kushiriki matembezi ya uzinduzi wa wiki ya sheria Mkoani humu, na kumhakikishia Mahakama katika Mkoa huo itaendelea kutoa elimu katika maeneo ya wazi pamoja na shuleni katika wilaya zote zilizopo Mkoani Songwe katika wiki hii ya sheria.
Maandamano ya uzinduzi wa Wiki ya utoaji elimu ya Sheria.
Katika picha ni Sajenti Wilfred Ruhega wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mkuu wa Kitengo cha uokoaji Mkoani Katavi akielezea vifaa mbalimbali vinavyotumika katika shughuli za uokoaji kwa mgeni rasmi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni