Na Tiganya Vincent-Mahakama -Dodoma
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ni
muhimu njia ya usuluhishi ili iweze kutatua migogoro kwa haraka inapotokea.
Rais
Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Februari 2023 katika Viwanja vya
Chinangali , jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria
nchini ambayo kauli mbiu yake ni; ‘Umuhimu wa utatuzi wa Migogoro
kwa njia ya Usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu: Wajibu wa Mahakama na
Wadau.’
Mhe.
Dkt. Samia amesema hatua hiyo itasaidia kuvutia na kulenga kuwajengea imani kwa
wafanyabiashara na wawekezaji juu ya usalama wa mali zao.
Ameongeza
kuwa, ni muhimu utaratibu wa usuluhishi ukapewa kipaumbele na uwe endelevu
katika kutatua migogoro ambayo haitaji wahusika kuwa wanasheria.
Aidha, Mhe. Dkt. Samia ameagiza kupitia taratibu na kuzifanyia marekebisho Sheria zote
zinazochelewesha kesi na upatikanaji haki ili zisiwe vikwazo katika kuharakisha
maendeleo nchini.
Ameongeza
kuwa ni vema mafunzo ya kusimamia taratibu za usuluhishi yakatolewa kwa vyombo
ambavyo vimepewa majukumu ya kusimamia usuluhishi ili wananchi wengi watumie
njia hiyo badala ya kukimbilia Mahakamani na kutumia muda mwingi na
gharama nyingi.
Wakati
huo huo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka viongozi
wa dini kutatua migogoro kwa njia usuluhishi kwa kuzingatia taratibu
zao badala ya kukimbizia masuala yao Mahakamani na kuanika siri zao.
Amesema
siku kizi kumeibuka tatizo la viongozi wa dini wanapokuwa na migogoro
kukimbilia Mahakamani badala ya kusuluhisha Katiba au Mabaraza yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya sheria nchini leo tarehe 01 Feberuari, 2023 katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma amesema ni muhimu kutumia njia ya usuluhishi ili kutatua migogoro kwa haraka inapotokea.
Meza Kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakati wa hafla ya kuadhimisha kilele cha siku ya sheria nchini.
Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu washuhudia gwaride la heshima lililokaguliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani) wakati wa shughuli ya kitaifa ya kuadhimisha kilele cha siku ya sheria nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni