Jumatatu, 4 Septemba 2023

RAIS SAMIA ATEUA MAJAJI WANNE MAHAKAMA YA RUFANI, 20 MAHAKAMA KUU

Na Faustine Kapama-Mahakama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua Majaji wanne wa Mahakama ya Rufani na wengine 20 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi Zuhura Yunus inaeleza uteuzi huo umeanza jana tarehe 3 Septemba, 2023.

Walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Lameck Michael Mlacha na Mhe. Paul Joel Ngwembe ambaye alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro.

Wengine ni Mhe. Mustafa Kambona Ismail, aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi na Mhe. Abdul-Hakim Amer Issa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar.

Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Mhe. Dkt. Evaristo Longopa, ambaye alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Wilbert Martin Chuma, aliyekuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Mhe. Sharmillah Said Sarwat, aliyekuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Wengine ni Mhe. Anold John Kirekiano, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Martha Mpaze, aliyekuwa Naibu Msajili Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Masuala ya Familia Temeke na Mhe. Ferdinand Hilali Kiwonde, aliyekuwa Naibu Msajili Mahakama Kuu.

Uteuzi mwingine ni Mhe. Said Rashid Ding’ohi, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha, aliyekuwa Naibu Msajili na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania na Bi. Sarah Duncan Mwaipopo, aliyekuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Wengine ni Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya, aliyekuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu, Dodoma, Bw. Griffin Venance Mwakapeje, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Wizara ya Katiba na Sheria Dodoma na Dkt. Dafina Daniel Ndumbaro, aliyekuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwenye orodha yupo pia Bw. Emmanuel Ludovick Kawishe, aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bw. Abdallah Halfan Gonzi, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Rufani za Kodi na Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaama.

Wengine ni Bw. Kamazima Kafananbo Idd, aliyekuwa Mhadhiri Msaidizi Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Bw. Frank Muyoba Mirindo, aliyekuwa Mhadhiri Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Bi. Hadija Ally Kinyaka, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili Lawhill Co. &Advocates.

Pia wapo Bi. Aisha Ally Sinde, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili BOWMANS Tanzania, Bw. Hussein Salum Mtembwa, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea na Mmiliki wa Kampuni ya Uwakili ya HM NOBLE Attorneys, Mtwara na Bi. Irene Daniel Musokwa, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea na Mshiriki katika Kampuni ya Uwakili ya FC Attoeneys.

Mhe. Lameck Michael Mlacha.
Mhe. Paul Joel Ngwembe.
Mhe. Wilbert Martin Chuma.
Mhe. Sharmillah Said Sarwat.
Mhe. Anold John Kirekiano.
Mhe. Martha Mpaze.
Mhe. Said Rashid Ding’ohi.
Mhe. Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni