Na Hassan Haufi-Mahakama, Songea
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani amewakumbusha wafanyakazi kuwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) haukuanzishwa ili kuchochea majanga kazini ili walipwe fidia.
Mhe. Siyani ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi kati ya Mahakama ya Tanzania na Mfuko huokilichoketi Februari 9, 2024 kanda ya Songea mkoani Ruvuma.
Aliongeza kuwa mfuko huo unapaswa kupunguza majanga yanayotokana na kazi kuliko fidia itakayotokana na madhara kazini.
Mhe. Siyani aliongeza kuwa kikao kitumike katika kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo yatakayoboresha maeneo muhimu katika sheria zinazolinda maslahi ya wafanyakazi na kwamba kufanya hivyo watakuwa wamewezesha kulindwa kwa haki za wafanyakazi.
Sambamba na hayo, Mhe. Siyani amewakumbusha watoa haki kujikomboa wenyewe kwenye minyororo inayowabana wakati wanapotimiza majukumu yao kwa kuwa jamii inawategemea zaidi wajikite kwenye utoaji haki za msingi.
Kikao kazi hicho ni cha nne kufanyika baada ya kikao cha kwanza Kanda ya Dar es Salaam, kikifuatiwa na vilivyofanyika Mwanza na Arusha, ambapo kilijumuisha Kanda za Mahakama Kuu Iringa, Mbeya, Mtwara, Songea na Sumbawanga, huku mafunzo mbalimbali kuhusu sheria za mfuko wa fidia kwa wafanyakazi yalitolewa.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi na Majaji wa Mahakama Kuu.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi nchini (CMA).
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na moja ya wanufaika wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni