Jumapili, 28 Aprili 2024

RAIS SAMIA AMWAPISHA JAJI KOROSSO KUWA MWENYEKITI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

  • Yumo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Aprili, 2024 amewaapisha Viongozi watatu katika nyadhifa mbalimbali, akiwemo Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Winfrida Korosso kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria. 

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wengine wakuu wa Kitaifa, akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma. 

Wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Hassan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi na wengine wengi.

Viongozi wengine walioapishwa ni Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,  Bi.Bibiana Kileo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,  Bi. Alice Mtulo.

Waapishwa hao waliteuliwa na Rais Samia kushika nyadhifa hizo tarehe 4 Aprili, 2024. Kabla ya uteuzi huo, Bi. Bibiana alikuwa Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mwanza na Bi. Alice alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti wa Ubora katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Winfrida Korosso akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria. 

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,  Bi.Bibiana Kileo akiapa kushika wadhifa huo.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,  Bi. Alice Mtulo akila kiapo kushika wadhifa huo.

Viongozi walioapishwa. Kutoka kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Winfrida Korosso ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Bi. Bibiana Kileo anayekuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka na Bi. Alice Mtulo anayekuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Sehemu ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliohudhuria uapisho huo. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Hassan Zungu na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka.

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi walioapishwa (waliosimama mstari wa nyuma).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni