Alhamisi, 4 Julai 2024

UJENZI WA MAHAKAMA TATU ZA MWANZO MKOANI LINDI WAIVA

Na HILARI GADIYE HERMAN- Mahakama, Lindi

Mahakama ya Tanzania imemkabidhi Mkandarasi kutoka Kampuni yaEngineering Plus’ viwanja vitatu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miradi mitatu ya Mahakama za Mwanzo mkoani Lindi.

Miradi hiyo itakayogharimu jumla ya shilingi Bilioni 3.5 za kitanzania inajumuisha mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi, Mahakama ya Mwanzo Mtandi iliyoko Wilaya ya Kilwa na Mahakama ya Mwanzo Ndomoni iliyopo Wilaya ya Nachingwea.

Akizungumza wakati wa makabidhiano miradi hayo hivi karibuni Mhandisi Mshauri Bw. Berno Batinamani alisema, ujenzi wa miradi ya Mahakama hizo tatu utachukua muda wa miezi sita (6) kwa mujibu wa mkataba hadi kukamilika kwake. Miradi hiyo unatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 13 Julai 2024 na kukamilika mnamo tarehe 12 Januari, 2025.

Aidha, Bw.Batinamani alitoa wito kwa Viongozi wa Vijiji vyote watakao nufaika na miradi hiyo kumpatia ushirikiano Mkandarasi huyo anayetekeleza ujenzi wa miradi hiyo ili aweze kuikamilisha kwa wakati. Aliongeza kuwa, miradi hiyo ni fursa kwa wanachi kwani nguvu kazi itahitajika wakati wa ujenzi wa miradi hiyo hivyo itawanufaisha kiuchumi.

Kwa upande wake Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Godfrey Mbeyela aliahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa pande zote zinazohusika na miradi hiyo, huku akiwataka Mhandisi Mshauri, Mkandarasi na viongozi wote wafanye kazi kama timu moja ili  zoezi la ujenzi likamilike kwa wakati.

Naye, Mkadiriaji Majenzi kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. Abdallah Nalicho alimtaka Mkandarasi kukamilisha kazi kwa wakati na kufuata vipengele vyote vilivyo ainishwa kwenye mkataba.

Nao, wananchi pamoja na viongozi kutoka vijiji vilivyonufaika na mradi wa ujenzi wa Mahakama hizo wamefurahishwa sana na miradi hiyo na kukiri kwamba miradi hiyo itawaondolea adha ya kufuata huduma za kimahakama umbali mrefu na kuongeza kuwa miradi hiyo itakuwa chachu ya maendeleo katika maeneo yao.

Makabidhiano ya miradi hiyo yalifanyika kati ya Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Qiup Godfrey Mbeyela na mwakilishi kutoka Kampuni ya ujenzi ya E-Plus Mhandisi Silas Paul huku yakishuhudiwa na Mkadiriaji Majenzi wa Mahakama Bw. Abdallah Nalicho, Mhandisi kutoka Mahakama Bw. Kelvin Juvinal na Mhandisi Mshauri Bw.  Berno Batinamani kutoka Kampuni ya Norman.

Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering Plus’  Mhandisi Silas Paul akionyeshwa mipaka na Mkadiriaji Majenzi wa Mahakama ya Tanzania Bw. Abdallah Nalicho (Aliyevalia reflector)



Makabidhiano ya Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama tatu za mwanzo Lindi kati ya Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering Plus’ Mhandisi Silas Paul na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela.

Makabidhiano ya Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama tatu za mwanzo Lindi kati ya Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering Plus’ Mhandisi Silas Paul na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela


Makabidhiano ya Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama tatu za mwanzo Lindi kati ya Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering Plus’ Mhandisi Silas Paul na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela

Mwenyekiti wa kikao cha makabidhiano ya eneo la mradi Bw. Berno Batinamani (aliyenyoosha mkono) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa mipaka.

Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering Plus’  Mhandisi Silas Paul akionyeshwa mipaka na Mkadiriaji Majenzi wa Mahakama ya Tanzania Bw. Abdallah Nalicho (Aliyevalia reflector)

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni