Alhamisi, 1 Agosti 2024

JAJI MFAWIDHI MPYA IRINGA ATETA NA WATUMISHI

  • Akemea majungu kazini

Na. LUSAKO MWANG’ONDA-Mahakama, Iringa

Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, Mhe. Dunstan Ndunguru amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa makini muda wote ili wananchi wanaridhike na huduma zinazotolewa na Mahakama. 

Mhe. Ndunguru, ambaye amehamia Mahakama Kuu Kanda ya Iringa hivi karibuni akitokea Mbeyaalikuwa anazungumza na watumishi kwa mara ya kwanza katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mahakama Kuu.

Katika hotuba yake, Jaji Ndunguru alisisistiza vitu vingi, ikiwemo ufanyaji kazi kwa kuzingatia maadili, kujiepusha na rushwa, kuheshimiana, umaridadi kwa kila mfanyakazi, utunzaji wa mazingira, umuhimu wa kijiendeleza kitaaluma na kufanya mazoezi kwa ajli ya kutunza afya.

Alisema kuwa ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya mtumishi yoyote kutoa mawazo na kushauri juu ya kitu chochote ilimradi kiwe ni kwa ajili ya kujenga, huku akisisitiza kuwa ofisi yake haitakuwa tayari kumpokea mtu mwenye majungu

“Mimi siyo muumini wa majungu majungu, ni bora usije ukiona jambo unalotaka kulileta kwangu ni kwa ajili ya kupika majungu juu ya mtu mwingine, maana siko tayari kusikiliza mambo ya kujunguana,” Jaji Ndungunru alisisitiza.

Jaji Mfawidhi Ndunguru amehamia Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kuchukua nafasi ya  Jaji Ilvin Mugeta ambaye amehamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, MheDunstan Ndunguru (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na watumishi wa Mahakama Kanda ya Iringa (hawapo pichani). Kushoto kwake ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mhe. Angaza Mwipopo na kulia kwake ni Jaji wa Mahakam Kuu Kanda ya Iringa, Mhe. Saidi Kalunde.

Sehemu ya watumishi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa wakimsikiliza Jaji Mfawidhi katika kikao hicho.

Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Bi. Doris Kisanga (aliyesimama) akisisitiza jambo  kwa watumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao hicho.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni