Jumatatu, 5 Agosti 2024

KIKAO CHA MAHAKAMA YA RUFANI MOSHI KUMALIZA MASHAURI 30

  • Rufani za jinai 15, madai 15 kuamuliwa ndani ya wiki tatu

Na. Paul Pascal-Mahakama, Moshi

Mahakama ya Rufani ya Tanzania hivi karibuni ilianya kikao na wadau wa mnyororo wa utoaji haki Mkoa Kilimanjaro ili kupanga mkakati wa kuanza usikilizwaji wa mashauri ya rufaa 30 kuanzia leo tarehe 5 Agosti, 2024.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Moshi kilijumuisha Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu Kanda Moshi, Naibu Msajili Mahakama ya Rufani, Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Moshi.

Walikuwepo pia Mawakili wa Serikali Mkoa wa Kilimanjaro, Mawakili wa Kujitegemea, Chapta ya Kilimanjaro, Ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro, Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na watumishi wa Mahakama.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Jopo hilo la kikao cha rMahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Mary Levira aliwaomba wajumbe kuweka mipango dhabiti wanapokwenda kuanza kazi ya kuwatumikia Watanzania katika utoaji haki.

“Kila mmoja wetu anayo nafasi yake muhimu kuhakikisha wananchi tunaowahudumia wanapata haki zao kwa wakati, hivyo tutumie muda huu kuweka ramani ya namna bora tutakayotumia katika kutimiza wajibu wetu, hii ni timu nzuri tutakwenda kufikia malengo yote tuliyokusudia,” alisema.

Majaji wengine wanaounda jopo la Mahakama ya Rufani Moshi ni Mhe Zephrine Nyalugenda Galeba na Mhe. Mustafa Kambona Ismail.

Jaji wa Mahakama ya Rufaani na Mwenyekiti wa jopo, Mhe. Dkt. Mary Levira akiendesha kikao na wadau (hawapo pichani)katika kuweka mkakati wa kumaliza rufaa ambazo zimepangwa kusikilizwa katika kikao. 

Naibu Msajili Mahakama ya Rufaa na Katibu wa Kikao, Mhe. Dayness Lyimo akichangia na kuelekeza mambo muhimu kwa wajumbe.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Lillian Mongella (wa kwanza kulia aliyevalia Miwani), Jaji wa Mahakama Kuu Moshi, Mhe. Safina Simfukwe (katikati) na Jaji wa Mahakama Kuu Moshi, Mhe. Adriani Kilimi wakifuatilia kikao hicho.

Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakifuatilia mada katika kikao hicho.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Sekela Mwaiseje (wa kwanza kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Mhe Oppoturna Kipeta na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mhe. Hud M Hud wakifuatilia uwasilishwaji wa maelekezo katika kikao hicho.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni