Jumanne, 6 Agosti 2024

MAHAKAMA YA RUFANI KUENDESHA VIKAO MAHAKAMA KUU SONGEA

Na. NOEL SYLIVESTER – Mahakama, Songea

Mahakama ya Rufani ya Tanzania inaendesha vikao vyake mjini hapa katika jengo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa za jinai na madai.

Vikao hivyo ambavyo vimeanza jana tarehe 5 Agosti, 2024 vinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 23 Agosti, 2024.

Katika Kanda ya Songea, vikao hivyo vitakuwa vikiendeshwa na jopo la Majaji watatu, ambao ni Mhe. Augustino Mwarija (Mwenyekiti), Mhe. Rehema Kerefu na Mhe. Omary Makungu. 

Vikao hivi vinafanyika sanjari na vikao vingine kwenye Kanda za Mwanza, Arusha, Tabora, Moshi na Dar es Salam na vyote vikiwa ni mwendelezo wa vikao vya Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2024.

Kabla ya kuanza kwa vikao hivyo kilifanyika kikao cha awali kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wakati wa kusikiliza rufaa za madai na jinai.

Kikao hicho kilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa Mahakama, wakiwemo Magereza, Polisi, Mawakili wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea.

 


Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Augustine Mwarija (katikati), Mhe. Rehema Kerefu (wa kwanza kushoto) na Mhe. Omary Makungu (wa kwanza kulia).

Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama ya Rufani, Mhe. Emmanuel Mrangu (aliyesimama).

Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea wakiongozwa na Jaji Mfawidhi, Mhe. James Karayemaha (wa kwanza kutoka kushoto) na Mhe. Emmanuel Kawishe (wa kwanza kutoka kulia).

Naibu Msajili Mahakama Kuu Songea, Mhe. Elizabeth Nyembere (aliyesimama).


Wadau waliohudhuria katika kikao cha awali.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni