Jumatatu, 5 Agosti 2024

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA MWANZO UYOLE MBEYA AFARIKI DUNIA

Marehemu Jackson Lutengano Msokwa enzi za uhai wake.

                                               TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza  kifo cha Mtumishi wake Bw. Jackson Lutengano Msokwa (katika picha) aliyekuwa  akihudumu Mahakama ya Mwanzo Uyole Mbeya  kwa Cheo cha  Msaidizi wa Kumbukumbu 

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Bi. Mavis Miti msiba umetokea usiku wa tarehe 03 Agosti 2024  kwa ajali ya kugongwa na Gari akiwa njiani kwenye pikipiki yake akielekea nyumbani kwake Mswiswi  Wilaya ya Mbarali. 

Bi. Mavis amesema mazishi yatafanyika tarehe 6 August 2024 katika kijiji cha Itende Kati.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba wa mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni