- Watoa pongezi kwa Viongozi na Watumishi kwa kazi nzuri inayofanyika
Na KENETH MNZAVA, Mahakama-Singida
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Jaji Mkuu ya Ufuatiliaji na Tathmini wamefanya ziara ya kutembelea Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao kama wajumbe wa Kamati hiyo.
Ziara hiyo ilianza tarehe 18 Novemba, 2024 wilayani Manyoni katika Mahakama ya Mwanzo Kintiku ambapo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania walipata fursa ya kukagua, kushauri, kuelekeza na kutoa pongezi pale ilipostahili.
Mara baada ya ukaguzi katika Mahakama ya Mwanzo Kintiku wajumbe wa Kamati hiyo walielekea Mahakama ya Wilaya Manyoni ili kuendelea na ukaguzi.
Aidha, tarehe 19 Novemba, 2024 Viongozi hao waliendelea na ukaguzi katika Mkoa wa Singida ambapo walianzia shughuli hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.
Katika ukaguzi uliofanyika Mahakama ya Wilaya Singida na Mahakama ya Mwanzo Utemini, Msajili Mkuu wa Mahakama, Mhe. Nkya aliwasisitiza Mahakimu kufuata sheria katika uzikilizwaji wa mashauri.
Aidha, alipongeza juhudi zinazofanywa katika kusikiliza na kumaliza mashauri kwa wakati ili kuondoa mashauri ya mlundikano.
Mara baada ya kumaliza ukaguzi kituoni hapo, wajumbe hao walielekea kukagua Mahakama ya Mwanzo Mjini Singida ambapo walipokelewa na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe.Said Siri Said.
Akiwa kituoni hapo, Msajili Mkuu aliwasitiza Mahakimu kuendelea kujisomea kutokana na mabadiliko ya sheria kubadilika mara kwa mara.
“Jengeni pia utamaduni wa kuelekezana kwa kuandaa mada tofauti tofauti na kuziwasilisha baina yenu, endeleeni pia kutumia fursa za mafunzo yanayotolewa kwa njia ya mtandao na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) ili kuboresha utendaji kazi wa kila siku,” amesema Mhe. Nkya.
Kwa upande wake Prof. Ole Gabriel alishauri kutunzwa kwa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuwekewa uzio ili kulilinda na uvamizi lakini pia kulihifadhi kwa matumizi ya baadaye pale ambapo shughuli za Mahakama hiyo zitakapohamia katika jengo jipya la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Singida kinachoendelea kujengwa.
Baada ya kukamilisha ukaguzi katika Mahakama hiyo, Viongozi hao walipongeza kazi nzuri ya utoaji haki inayofanyika katika Mahakama hiyo.
Kadhalika, Mtendaji Mkuu pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kwa pamoja walipata fursa ya kufika na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo jumishi (IJC) unaondelea Mkoani Singida.
Wakiwa katika ukaguzi wa Mradi huo, Prof. Ole Gabriel alimsisitiza Mkandarasi kufanya kazi kwa bidii na kwa ubora unaotakiwa ili mradi huo ukamilike kwa wakati kama makubaliano ya mkataba yanavyosema.
Matukio katika picha ya ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Jaji Mkuu ya Ufuatiliaji na Tathmini-Singida.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.Prof Elisante Ole Gabriel(kulia) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe.Eva Kiaki Nkya wakisaini vitabu vya wageni walipowasili katika Ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyeketi mbele) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (aliyeketi katikati) wakiwa katika ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kintiku Mhe. Faraja Kombe (kushoto). Wamempongeza Hakimu huyo kwa kutokuwa na mashauri ya mlundikano.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati)pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (wa pili kushoto) wakiwa katika ukaguzi katika Mahakama ya Mwanzo Kintinku.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.Prof.Elisante Ole Gabriel akipokelewa na kusalimiana na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Manyoni mara baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na Msajili Mkuu kwa ajili ya ukaguzi wa Mahakama hiyo.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (wa kwanza kushoto) akisaini kitabu cha wageni. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Afisa kutoka Idara ya Ukaguzi na Usimamizi wa Maadili. Anayezungumza ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Manyoni, Mhe.Alisile Mwankejela akiwakaribisha wajumbe hao.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.Eva Kiaki Nkya (aliyesimama) akitoa salamu za pongezi kwa watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Manyoni pamoja na Mahakama ya Mwanzo Mjini katika ukumbi wa wazi wa Mahakama hiyo mara baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof.Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Manyoni. Aliwasisitiza watumishi hao kupendana na kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano, aliwapongeza pia kwa namna wanavyolitunza jengo hilo jipya na kuendelea kusisitiza juu ya utunzwaji wa rasilimali zilizopo.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.Prof.Elisante Ole Gabriel (wa tatu kushoto) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.Eva Kiaki Nkya (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Manyoni na Mahakama ya Mwanzo Mjini baada ya kumaliza kuzungumza na watumishi hao hivi karibuni.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe. Prof Elisante Ole Gabriel (wa sita kulia) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe.Eva Kiaki Nkya (wa saba kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.
Wajumbe wa Kamati ya Jaji Mkuu ya Tathmini na Ufuatiliaji wakiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe.Silivia Lushasi (wa tatu kushoto). Wajumbe hao walipata fursa ya kusalimiana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mhe.Suleiman Hassan anayeendelea na vikao vya Mahakama Kuu katika Mahakama ya Wilaya iliyopo katika jengo la Mahakama ya Mwanzo Utemini.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof.Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Mahakama ya Mwanzo Utemini. Katikati ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.Eva Kiaki Nkya akimsikiliza kwa ukaribu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma, Mhe.Silivia Lushasi (kushoto) alipokuwa akizungumza nae.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe.Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akiwasalimu watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mjini huku akiongozwa na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu ya Mwanzo Mjini, Mhe.Said Siri Said.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) na Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe.Eva Kiaki Nkya (wa pili kushoto) wakiwa sehemu ya juu ya jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) kinachojengwa mkoani Singida.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof.Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) na Msajili Mkuu wa Mahakama Mhe.Eva Kiaki Nkya (wa kwanza kushoto) wakikagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Singida wakiwa wameongozana na Wakandarasi wa Mradi huo.
(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni