Alhamisi, 16 Januari 2025

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA

 TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Marehemu Winnie Wakili Mwangoka aliyekuwa akihudumu kama Hakimu Mkazi Daraja la Pili katika Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga Mjini.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Marehemu Winnie Wakili Mwangoka alianza kuumwa toka mwaka 2022. Alipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga na baadae Hospitali ya Rufaa Mbeya na vilevile alipata matibabu katika Hospital ya Taifa Muhimbili (Ocean Road Cancer Institute). Hadi umauti unamkuta mnamo majira ya jioni ya tarehe 15 Januari, 2025 alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.

Marehemu Mwangoka aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania mnamo tarehe 18 Februari, 2021. Alipangiwa kufanya kazi Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Sumbawanga Kituo cha Laela. Na mnamo Mwezi Septemba, 2023 alihamishiwa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Sumbawanga Kituo cha Sumbawanga Mjini.

Taarifa nyingine kuhusu mazishi ya msiba huu, zitazidi kutolewa kadri muda utakavyokwenda.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBAKIRIWE


Marehemu Winnie Wakili Mwangoka enzi za uhai wake.

Maoni 2 :

  1. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake na amsamehe makosa yake nankumpokea kwenye ufalme wake.

    JibuFuta
  2. Mungu amweke mahali pema peponi!

    JibuFuta