Jumamosi, 8 Machi 2025

MAADHIMISHO SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE WATUMISHI WAINOGESHA

Na INNOCENT KANSHA- Mahakama

Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota, leo tarehe 8 Machi, 2025 amewaongoza Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Tanzania, Makao Makuu ya Mahakama kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyofanyika katika Jengo la Makao Makuu jijini Dodoma.

Akifungua hafla ya maadhimisho hayo Bi. Kipobota amechukua furusa hiyo kuwapongeza watumishi hao kwa kujitoa kushiriki hafla hiyo licha ya kuwa na ratiba ngumu ya majukumu ya kiofisi na kifamilia na hasa ikizingatiwa kipindi hicho ni cha mfungo wa Kwaresma na Ramadhan.

“Ni heshima kubwa kuungana kwa pamoja watumishi wanawake wa Mahakama ya Tanzania Makao Makuu kusherekea siku hii muhimu inayotukumbusha mambo mengi ya ustawi wa mwanamke kiuchumi, kijamii, kiafya na hata kisiasa kwani mwanamke akielimika jamii inakuwa imejikomboa,” alisema Mkurungenzi huyo.

Bi. Kipobota ameongeza kuwa, Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 1911 yakiwa na lengo Kuu la kuikumbusha jamii kuhusu haki na umuhimu wa mwanamke katika jamii inayomzunguka.

“Siku ya leo na uwepo wetu mahali hapa unadhihirisha ni kwa namna gani wanawake wa Mahakama tupo mstari wa mbele katika kutambua haki zetu, kujiinua kiuchumi ili kuleta usawa katika Mhimili, familia zetu na jamii kwa ujumla,” amesisitiza Bi. Kipobota.

Dhima ya maadhimisho ya siku ya wanawake kwa mwaka huu ni Wanawake na wasichana 2025: Tuimarishe Haki, usawa na Uwezeshaji”. Dhima hiyo, inawakumbusha wanawake wote waliopo Mahakama ya Tanzania kujiuliza maswali kwa nafasi zao mmoja mmoja. 

“Je? tumefanikiwa kutoa haki kwa wanawake wenzetu wanaofika kupata huduma Mahakamani kwa kiasi gani? na Je? dhana ya usawa katika maamuzi na utendaji kazi wetu tunaizingatia ipasavyo au bado baadhi yetu tuna mitazamo ya mila potofu dhidi ya mwanamke?,” aliwataka wanawake wa Mahakama kutafakari kwa makini mchango wao kwa jamii inayowazunguka. 

Akitoa takwimu za mchango wa wanawake katika masuala ya usawa, Mkurugenzi Beatrice amesema, takwimu zinaonyesha Mahakama ya Rufani na  Makao Makuu ya Mahakama ina jumla ya wanawake 198 ambao miongoni mwao wapo Majaji, Naibu Wasajili, Wakurugenzi, Mahakimu, Wasaidizi wa Sheria wa Majaji, Wakuu wa Vitengo na watumishi wa kada zingine.

“Umahiri wetu unatokana na kushirikiana na Watumishi Wanaume  tunatekeleza jukumu zima la utoaji haki kwa wananchi kwa wakati. Hivyo, nitoe rai kwa watumishi wenzangu wanawake kuendeleza juhudi katika utoaji haki kwa jamii na mahali pa kazi na bila kuziacha nyuma familia zetu,” amesisitiza Mkurugenzi huyo. 

Aidha, takwimu zilizopo kwa sasa zinaonesha kwamba, katika Mhimili wa Mahakama kuna usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za Uongozi. Mathalani kuna Majaji wa Mahakama ya Rufani 39 ambapo wanawake ni 13 sawa na asilimia 33, Majaji wa Mahakama Kuu wako 104 wanawake ni 40 sawa na asilimia 38, Naibu Wasajili wako 82 wanawake ni 42 sawa na asilimia 51 na Watendaji wa Mahakama wapo 42 wanawake wako 9 sawa na asilimia 21.

“Wanawake tunatakiwa kujivunia mafanikio hayo na kuendeleza juhudi ili uwezo wetu uonekane katika utendaji kazi wetu. Halikadhalika, napenda kutoa wito kwa wanawake wenzangu kuendelea kuhakikisha tunahamasisha masuala ya haki na usawa kwa jamii bila kusahau watu wenye mahitaji maalum,” amesema kwa bashasha Mkurugenzi Kipobota.

Mkurugenzi huyo akatoa wito kwa kuwaomba wanawake hao kuishi kwa kupendana, kuinuana na kusaidiana hivyo kuwa daraja la mafanikio kwa wanawake wengine hasa kwenye maeneo yao ya kazi na hata nje ya kazi.

“Tuendelee kuiomba Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania kuendelea kutuamini na kutuwezesha kushika nafasi mbalimbali za Uongozi na kutoa fursa mbalimbali zitakazotufanya tutumie utaalamu, ujuzi, maarifa na weledi tulionao katika kutekeleza majukumu yetu kazini na kusaidia jukumu la utoaji haki kwa wananchi na hivyo kusaidia kufikia dira, dhima na malengo ya Mahakama,” amesema Mkurugenzi.

Mkurugenzi Kipobota amesema kupitia hafla hiyo watumishi wanawake watapata ujuzi na elimu kutoka kwa wataalam watakao mada muhimu kabisa kuhusiana namna mwanamke anavyoweza kuwekeza ili  kujikwamua kiuchumi. Kadhalika kupata elimu itakayosaidia katika kuwaweka sawa kiakili na kiafya na hivyo kuimarisha utendaji kazi maofisini na kwa familia.

“Ni imani yangu  kwamba, elimu hii tutakayopata itatusaidia sisi binafsi na tutaweza kuifikisha kwa jamii nzima inayotuzunguka kutokana na nguvu ambayo Mungu aliweka ndani yetu Wanawake,” amesisitiza Bi. Kipobota.

Kwa upande wake, mtoa Mada ya namna mwanamke anavyoweza kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Hawa Mnguruta amesema yapata miaka 30 sasa toka maazimio ya Beijing China ndiyo yaliyochangia kwa kiasi kikubwa kuleta ukombozi wa mwanamke kiuchumi. Katika miaka hiyo 30 mambo mengi yameshafanyika mfano; katika uongozi wa ngazi ya juu kabisa Tanzania inaongozwa na Rais Mwanamke hayo ni sehemu ya mafanikio ya mwanamke kiuchumi.

“Kwenye mbinu za haki na usawa moja wapo ya kitu cha msingi ni uchumi kupitia ajira na uwekezaji mwingine, ukiwa mama wa nyumbani haki hizo na usawa hutaviona kwasababu kuna mambo itabidi uyafanye kutokana na uchumi kutokuwa imara, mfano; mwanamke huyo angetani kufanya kitu flani lakini anabaki kujilaumu ingelikuwa hivi ningefanya vile,” amesema Naibu Msajili huyo.

Mhe. Mnguruta amesema, njia moja wapo ya kujikomboa kiuchumi kwa mwanamke ni kuwekeza kwenye Taasisi ya kifedha ya umma iliyo chini ya Wizara ya Fedha mfano; ‘Unit Trust of Tanzania’ (UTT) ambao masharti yake sio magumu kwa mtu kuwekeza hata awe mwanamke mwenye kipato kidogo.

“Bila kudhamiria kuweka akiba hautaweka hakiba, jijengeeni utamaduni wa kuweka akiba kidogo kidogo wasahili wanasema bandu bandu humaliza gogo la asali. Nitoe rai kwa wanawake wenzangu kutumia mfuko huu kuwekeza pesa kidogo kidogo kadri unavyojaliwa na mwisho wa siku itakuwa mkombozi wa maisha yako na familia yako, kwani uwekezaji huu ni mzuri na rahisi sana,” amesema Mhe. Mnguruta.

Naye, Mtaalum wa masuala ya Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Magonjwa ya Akili Mirembe jijini Dodoma Dkt. Sadick Mandari amewaasa wanawake kupata muda wa kutosha wa kupumzika mara baada ya kutoka kazini kawaida mtu anapaswa kulala kati ya masaa saba hadi nane ili kuepuka msongo wa mawazo na kuondoa sonona, kwani mambo hayo yanaweza kuathiri afya ya akili.

Dkt. Mandari amesema kwamba, mambo ya kuzingatia ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya ya akili ni pamoja na tukio kama hilo la maadhimisho ya Siku Wanawake kitaifa, kupata muda wa kukutana na kufurahi kwa pamoja mara kwa mara, kula chakula bora na siyo bora chakula, kulinda afya ya uzazi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kutembelea mbuga za wanyama na vivutio vingine vya asili na kupata muda wa kukaa kwanye sehemu yenye utulivu na pia kutotumia vilevi kama pombe kupita kiasi.

“Ukiweza kuepuka mambo hayo inaweza kukusaidia kuepuka mambo yanayoweza kuathiri afya ya akili na kukujengea utimamu wa afya ya akili katika maisha yako yote,” aliongeza Mtaalum huyo.

Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota, akifungua hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wa Makao Makuu ya Mahakama leo tarehe 8 Machi, 2025, hafla  iliyofanyika katika Jengo la Makao Makuu jijini Dodoma

Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota, akisisitiza jambo wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Watumishi Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wa Makao Makuu ya Mahakama leo tarehe 8 Machi, 2025, hafla  iliyofanyika katika Jengo la Makao Makuu jijini Dodoma.

Mtoa Mada ya namna mwanamke anavyoweza kuwekeza ili kujikwamua kiuchumi, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Hawa Mnguruta akiwasilisha mada hiyo kwa watumishi wanawake wa Mahakama (hawapo pichani).

Mtaalum wa masuala ya Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Magonjwa ya Akili Mirembe jijini Dodoma Dkt. Sadick Mandari akiwasilisha mada ya Afya ya akili kwa watumishi Wanawake wa Mahakama wa Makao Mkuu ya Mahakama (hawapo pichani).

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wanawake wakati wa hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wanawake wakati wa hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wanawake wakati wa hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wanawake wakati wa hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wanawake wakati wa hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota akipongezana na watumishi wanawake wa Mahakama kwa kugongesheana glasi kama ishara ya upendo na umoja.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota akipongezana na watumishi wanawake wa Mahakama kwa kugongesheana glasi kama ishara ya upendo na umoja.

 Sehemu ya watumishi wanawake wa Mahakama wakinyanyua glasi juu ikiwa ni ishara ya kupongezana wakati wa hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.



Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota akishirikiana na mwakilishi wa watumishi wanawake kukata keki kama ishara ya maadhimisho hayo.

Mkurungenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick Kipobota (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo Mahakama ya Tanzania Bi. Patricia Ngungulu (kushoto)






Watumishi wanawake wa Mahakama ya Tanzania Makao Makuu ya mahakama jijini Dododma wakiselebuka na kwaito.


Watumishi wanawake wa Mahakama ya Tanzania Makao Makuu ya mahakama jijini Dododma wakiselebuka na kwaito






  Sehemu ya Watumishi wanawake wa Mahakama ya Tanzania, Makao Makuu ya Mahakama jijini Dododma  wakiomba Dua kabla ya kuanza hafla ya maadhimisho hayo.

(Picha INNOCENT KANSHA - Mahakama)


 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni