Na EUNICE LUGIANA-Mahakama, Pwani
Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam hivi karibuni walipata IFTAR kwa pamoja, jambo linalolenga kudumisha ushirikiano kwa kada zote.
IFTAR hiyo ulifanyika na kuhudhuriwa na Majaji wote wa Kanda hiyo pamoja na Watumishi wa kada mbalimbali.
Akiwakaribisha Watumishi katika IFTAH hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. SalmaMaghimbi alimshukuru Mungu kwa kuwapa kibali tena cha kufikia funga ya mwaka.
Aliomba pia Mungu aendelee kuwalinda na kuwapa uhai na kuwarehemu katika funga hizi mbili ya Ramadhani na Kwaresma.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa radhi zake tukawa hai mpaka sasa hivi na tumuombe kwa rehema za mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma atuondoshee balaa na husda na kila aina ya baya katika kazi zetu na atufungulie mioyo yetu na akili zetu ukawe mwaka wenye heri kama ulivyokuwa mwaka ambao umepita,” alitoa dua hiyo Mhe. Maghimbi.
Kwa miaka miwili funga ya Kwaresma na Ramadhan zimekutana kwa pamoja, hivyo kuwezesha kuandaa IFTAH ya pamoja kwa Wakristo na Waislamu.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi-wa pili kulia-akiwa na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya IFTAH.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Moses Mashaka (kushoto) akiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Kanda ya Dar es Salam, Mhe. Livin Lyakinana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mhe. Is-haq Kuppa pamoja na Mtendaji wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Kinondoni, Bw. Beatus Mlando.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni