Na AIDAN ROBERT, Mahakama-Kigoma
Viongozi wa
Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hivi
karibuni, kwa nyakati tofauti, walimtembea Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Augustine Rwizile, kwa nia ya kukuza ushirikiano
wa kitaasisi katika maeneo ya kusimamia sheria za uhamiaji na kutoa haki kwa
jamii ya watu kutoka nchi hizo mbili.
Balozi Mdogo wa Burundi Kigoma, Mhe. Kekenwa Jeremie aliishukuru Mahakama Kuu Kigoma
na Mahakama zake za chini kwa kuwahudumia vyema Wananchi kutoka nchini kwake wanaopata
changamoto ya kuingia Tanzania bila kibali.
‘Wananchi
kutoka Burundi wamekuwa wakipata haki zao za adhabu na kurudishwa Burundi na
kuwa funzo kwa wengine ambapo wimbi hilo linaendelea kupungua, watu wetu wengi
wanafuata taratibu za kuingia nchini Tanzania,” alisema.
Aliendelea
kusisitiza kuwa Serikali ya Burundi inatambua kazi nzuri inayofanywa na
Mahakama Kuu Kigoma kupitia huduma ya kisheria wanayopewa Wananchi toka Burundi
wanapofikishwa katika Mahakama hizo, moja ikiwa ni haki ya kupata mtafsili wa
lugha toka Kiswahili kwenda Kirundi, ili Mshatakiwa aweze kufahamu vema kosa
pamoja na mwenendo mzima wa shauri lake mahakamani.
Balozi Mdogo wa Kongo Kigoma, Mhe. Kinyamba Kitambe Louis, alipomtembelea Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Kigoma naye aliipongeza Mahakama Kanda ya Kigoma kwa kazi nzuri ya kutoa haki kwa watu wake kutoka Kongo wanapopatwa na chanagamoto za kuingia nchini bila kibari.
‘Hakika
tumekuwa tukipata taarifa njema ubalozini kuhusu kazi ya Mahakama kwa namna
mnavyotoa haki kwa watu wetu, hata hivyo kuja hapa nikuomba ushirikiano huu
udumu zaidi ili kuwasaidia watu wetu kuishi kwa kufuata sheria,” alisema.
Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi alipokea pongezi hizo kwa niaba ya Watumishi wote wa Mahakama Kanda ya Kigoma, alisema, ‘Nimepokea pongezi hizi kutoka kwenu, ni kweli kwamba Taasisi yetu inafanya kazi kwa mjibu wa sheria na taratibu mbalimbali ili kuhakikisha haimuonei mtu wa nchi yoyote na haki yake haichelewi kutolewa kwake.”
Mhe. Rwizile alitumia fursa hiyo kuwapa pole Viongozi na Wananchi wa Kongo kwa vita inayoendelea nchini humo kwa watu kupoza uhai wao na mali zao pia.
Mazungumzo hayo yalihudhuliwa na Viongozi wa Mahakama, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Mhe. Fadhili Mbelwa na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Bw. Filbert Matotay.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Augustine Rwizile (kulia) akisalimia na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kigoma, Mhe. Kinyamba Kitambe Louis, mara baada ya Balozi huyo na ujumbe wake kuwasili katika Ofisi ya Jaji Mfawidhi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Augustine Rwizile (kulia) akifafanua jambo wakati wa maongezi na Balozi Mdogo wa Burundi Kigoma, Mhe. Kekenwa Jeremie.
Picha ya pamoja Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Augustine Rwizile (wa pili kulia) na wa tatu kushoto ni Balozi Mdogo wa Burundi Kigoma, Mhe. Kekenwa Jeremie (kulia). Wengine ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Mhe. Fadhili Mbelwa (kushoto), wa kwanza ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Bw. Filbert Matotay.
Picha ya pamoja Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Augustine Rwizile, (wa tatu kulia) na wa nne kushoto ni Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kigoma, Mhe. Kinyamba Kitambe Louis. Wengine kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Mhe. Fadhili Mbelwa na wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Bw. Filbert Matotay.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni