Na Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya
Baraza
la wafanyakazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya lilikutana na kufanya
kikao cha kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu watumishi kikiwa na lengo la
kukumbushana na kuelimishana misingi ya kufanya kazi kwa ushirikiano tarehe 03
Aprili, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Mahakama Kuu Mbeya.
Akifungua
kikao cha Baraza hilo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo
aliwasisitiza watumishi mkoani humo kudumisha ushirikiano miongoni mwao,
kufanya kazi kwa uadilifu na kufanya kazi kwa bidii kwani ndiyo lengo kuu la
kuwakutanisha na kukumbushana majukumu ya kila siku.
“Ni
matumaini yangu kuwa tutayaishi haya tunayokubaliana hapa, mkafanye kazi kwa
bidii na uadilifu lakini pia tusisahau kuwa ushirikiano baina yetu ni muhimu na
unajenga mshikamano na kuleta matokeo chanya katika utendaji wetu wa kazi,”
alisema Jaji Tiganga
Aidha
katika baraza ilo hoja mbalimbali za watumishi zilipokelewa na kujadiliwa na
ambazo zilihitajika kuchukuliwa zilichukuliwa, watumishi walishukuru uongozi
kwa kuwepo kwa Baraza hilo na hoja zao kusikilizwa.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akifungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi Kandaya ya Mbeya tarehe 03 Aprili, 2025 katika ukumbi wa mikutano Mahakama Kuu Mbeya.
Sehemu
ya Wajumbe wa kikao hicho cha baraza la wafanyakazi wakiimba wimbo wa
solidarity forever.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni