Na Mwinga Mpoli –
Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles
Tiganga amewahimizwa Mahakimu kuhusu suala la usikilizaji na umalizaji wa
mashauri kwa wakati na matumizi sahihi ya mifumo ya Mahakama lakini pia
kuhakikisha wanaepuka kujaza mahabusu magereza ambao wana haki kudhaniniwa kwa mujibu
wa sheria.
Mhe.
Tiganga aliyasema hayo hivi karibuni katika kikao cha menejementi ya Kanda ya
Mbeya kilichojumuisha Mkoa wa Mbeya na Mkoa Songwe na kusisistiza kufuata
miongozo, kanuni, sera na sheria zilizopo ili kufanikisha utendaji kazi kwa
ueledi na ufanisi wakati wa utoaji haki kwa wananchi.
“Tukumbuke
kuwa tunalojukumu la kuhakikisha tunasikiliza mashauri na kuyamaliza kwa
wakati. Aidha tuepuke kupeleka watuhumiwa mahabusu na magereza ambao wanaweza
kupata dhamana au adhabu mbadala. Pia niwakumbushe tunapaswa kuhakikisha tuna
matumizi sahihi ya mifumo yetu na kuwa tunaipitia mara kwa mara ili tuweze
kutathmini utendaji kazi wetu,” alisema Jaji Tiganga.
Aidha,
Mhe. Tiganga aliwasisitiza juu ya kusimamia utekelezaji wa mashauri na kama
kutakuwa na changamoto wahakikishe wanatumia ubunifu ili kuhakikisha hawakwami
katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kikao
kazi hicho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka mkoa wa songwe na Mbeya ambao kwa pamoja
wanaunda Kanda ya Mbeya.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akieleza
jambo katika kikao hicho.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga (katikati)
kulia ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza
Emily Temu na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Mbeya Bi Mavis Miti katika
kikao hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni