Jumatatu, 14 Aprili 2025

JAJI MKUU ASAFIRI KWA SGR HADI MOROGORO

Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Morogoro.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 14 Aprili, 2025 amewasili mjini hapa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania-JMAT.

Mhe. Prof. Juma aliwasili katika Stesheni ya Jakaya Kikwete Morogoro majira ya saa 10.15 jioni kwa kutumia Reli ya Mwendokasi-SGR akitokea jijini Dodoma na kupokelewa na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro pamoja na Viongozi wengine.

Alikuwepo pia Meneja Msaidizi wa Stesheni ya Jakaya Kikwete Morogoro, Bi. Getruda Masanja. Baada ya kufika katika Stesheni hiyo, Jaji Mkuu aliongozwa katika Chumba cha Watu Mashuhuri na kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye sehemu ambayo ameandaliwa kwa mapumziko.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Morena leo tarehe 15 Aprili, 2025 utafungulia na Mhe. Prof. Juma ambaye ndiye mgeni rasmi. Wakati wa Mkutano huo, wajumbe watajadili mambo mbalimbali na kuchagua Viongozi wapya.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akishuka kwenye Treni ya SGR katika Stesheni ya Jakaya Kikwete Morogoro kuhudhuria Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania. Picha chini ni Treni ya SGR.




Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma-kushoto-akisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma. Picha chini akiteta jambo na Majaji hao.





Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma-kushoto-akisalimiana na Meneja Msaidizi wa Stesheni ya Jakaya Kikwete Morogoro, Bi. Getruda Masanja.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma-kushoto-akiongozwa kuelekea kwenye chumba cha watu mashuhuri-juu na picha mbili chini.

 



Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma-kushoto-akisaini kitabu cha wageni. Picha chini akizungumza machache na Meneja Msaidizi wa Stesheni ya Jakaya Kikwete Morogoro, Bi. Getruda Masanja.



Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiondoka katika Stesheni ya Jakaya Kikwete Morogoro-picha chini.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni