Jumatatu, 14 Aprili 2025

JAJI MKUU, JAJI KIONGOZI WATUA MOROGORO KWA TRENI YA UMEME

Na ASHA JUMA-Mahakama, Morogoro.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewasili mkoani Morogoro kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu (JMAT) utakaofanyika siku ya Jumanne tarehe 15 April 2025 katika ukumbi wa Morena Hotel.

Jaji Mkuu amewasili na treni ya umeme, maarufu SGR kutokea jijini Dodoma majira ya saa 10:15 akipokelewa na mwenyeji wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Rose Ebrahimu na Majaji na Mahakimu wa Mahakama Kanda ya Morogoro.,

Aidha, Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro imempokea Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt Mustapher Mohamed Siyani, ambaye pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

Mkutano wa Chama cha Mahakimu na Majaji unatarajia kufanya uchaguzi wa kupata viongozi wa chama hicho kama vile Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makatibu katika ngazi za juu za chama hicho.

Mkutano huo ambapo awali ulitarajiwa kufanyika December 2024 ulisogezwa mbele kupisha mkutano mkuu wa Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki.


 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwasili mkoani Mororgoro kwa treni ya umeme maarufu SGR kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni katika stesheni ya Jakaya Kikwete alipowasili kuhudhuria mkutano huo.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Rose Ebrahim alipowasili mkoani hapa.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Meneja Msaidizi wa Stesheni ya Jakaya Kikwete, Bi. Getruda Masanja.

Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt, Mustapher Mohamed Siyani akiwasili mkoani Morogoro kuhudhuria mkutano wa Majaji na Mahakimu utakaofanyika Morena Hotel Jumanne tarehe 15 April 2025.

Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt, Mustapher Mohamed Siyani akisaini kitabu cha wageni katika stesheni ya Jakaya Kikwete Mororgoro.

Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt, Mustapher Mohamed Siyani akipokewa na Majaji na Mahakimu wa Mahakama Kuu Kanda ya Mororgoro.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Morogoro.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni