Alhamisi, 10 Aprili 2025

PROF. OLE GABRIEL; POSHO KWA WATUMISHI SASA SIYO NDOTO TENA

Na INNOCENT KANSHA-Mahakama

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa rai kwa watumishi kuendelea kuwa watulivu, wavumilivu, kuonyesha mshikamano na kufanya kazi kwa bidii wakati Mahakama kupitia ofisi hiyo ikichukua hatua stahiki za kushughulikia kero mbalimbali za watumishi.

Akiwasilisha taarifa katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama la mwaka 2025, liloanza vikao vyake vya siku mbili kuanzia leo tarehe 10 hadi 11 Aprili, 2025 jijini Dodoma, Prof. Ole Gabriel amesema maslahi ya watumishi ni jambo linalopewa kipaumbele, yaliwasilishwa maombi ya watumishi ya malipo ya posho mbalimbali, baadhi ya maombi hayo yamefanyiwa kazi na tayari yaingizwa kwenye bajeti, mengine yanaendelea kufanyiwa kazi na mengine hayatawezekana kutekelezeka kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Taasisi.

Aidha, Mtendaji Mkuu amesema kuwa, Posho hizo zilizopitishwa zitaanza kutumika katika mwaka mpya wa fedha 2025/26, posho hizo ni pamoja na posho ya kutotumia utaaluma kwa ajili ya Maafisa Mahakama (Non Practising allowance), Mtendaji Mkuu akafafanua kuwa, posho hiyo ni maalumu kwa ajili ya Majaji na Mahakamu wote, Posho nyingine ni ya Mavazi kwa ajili ya Majaji na Mahakimu (Court attire) posho hiyo ipo kwa mujibu wa sheria hivyo ni lazima itekelezwe.

“Na tunapozungunzia unifomu kwa ajili ya kada zingine ni utaratibu mwingine wa posho ya mavazi hadi sasa Mahakama imefanikiwa kutoa posho hizo kwa watumishi wa kada za Waandishi waendesha Ofisi, Walizi, Maafisa Usafirishaji (Madereva). Viwango vya posho hizo havifanani kutokana na sababu mbalimbali zilizoainishwa kiutumishi. Aidha, niwaombe wale ambao pengine hawapati sawa kama wasaidizi wa kumbukumbu tuendelee kuwa wavumilivu tutaendelea kuongeza posho hizo kadri taratibu zitakapo ruhusu,” amesema Prof. Ole Gabriel.

Vilevile, Mtendaji Mkuu ameongeza kuwa aina nyingine ya posho ni kwa ajili ya bando (Data allowance), posho hiyo ni maalum itaanza kutumika kuanzi mwezi Julai mwaka 2025, itahusisha kada zote za chini vile, kada ya Wasaidizi wa Kumbukumbu (Makalani) ambao wapo takribani 1,324 kwa nchi nzima watalipwa posho hiyo kila mwezi, kada nyingine ni Waandishi waendesha Ofisi nao watafanyiwa hivyo hivyo.

Lakini pia kulikuwa na ishu ya posho za nauli kwa Madereva wanaowaendesha Waheshimiwa Majaji na Mahakimu mambo hayo yana umaalum wake licha ya kwamba kwa sasa wanapewa posho kidogo ya nauli, kuna baadhi yao wanaondoka na magari, hoja hiyo imechukuliwa na inafanyiwa kazi, hoja nyine ni posho ya chakula ambayo Mtendaji Mkuu amesema kwa sasa Mahakama haijamudu kuwahudumia watumishi wote ila akashauru kama kuna Kanda zinaweza kufanya hivyo kupitia bajeti za watendaji wao basi wanaweza kufanya hivyo.

Mtendaji Mkuu huyo akagusia suala la ujenzi wa makazi ya watumishi ingekuwa ni jambo jema hasa maeneo yenye jiografia zenye ukakasi lakini kwa bahati mbaya uwezo huo kwa sasa bajeti ya Mahakama hairuhusu kwa kiasi kikubwa Mahakama imefanikiwa kujenga nyumba 48 za majaji za daraja la kwanza jijini Dodoma eneo la Iyumbu Complex, nyumba hizo zina thamani ya shilingi bilioni 42.5.

Mara baada ya kukamilisha miradi wa kujenga nyumba za makazi ya majaji kwa maeneo mengine nchini tutaanza kuwaangalia na Mahakimu “kuna maeneno mengine yanaukakasi kwa mfano ukienda kusini kule kama vile Nanjilinji ni maeneo ambayo hata kupata nyumba yenye hadhi ya hakimu ni kazi kidogo. Hivyo basi miradi itatekelezwa hatu kwa hatua tunaomba watumishi tuvumiliane ili kuifikia hiyo ndoto,” amesema Mtendaji Mkuu.

Kuhusu hoja za uhamisho wa watumishi waliohama na hawajalipwa stahiki zao, Prof. Ole Gabriel amesema, kama taarifa ilivyoonyesha kwenye utekelezaji Mahakama inawahidi watumishi kuwa itaendelea kulifanyia kazi na watumishi watapata stahiki zao. Akitoa mfano amesema kuna watumishi 38 kati yao ni Mahakimu Wakazi 28 wanadai shilingi milioni 519 taarifa zao zinahakikiwa na watalipwa kabla ya mwaka wa fedha kuisha.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za watumishi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama la mwaka 2025, liloanza vikao vyake vya siku mbili kuanzia leo tarehe 10 Aprili, 2025 jijini Dodoma. 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za watumishi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama la mwaka 2025, liloanza vikao vyake vya siku mbili kuanzia leo tarehe 10 Aprili, 2025 jijini Dodoma. 

Sehemu ya wajumbe kutoka Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama la mwaka 2025, liloanza vikao vyake vya siku mbili kuanzia leo tarehe 10 Aprili, 2025 jijini Dodoma. 
Sehemu ya wajumbe kutoka Kanda ya Dodoma katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama la mwaka 2025, liloanza vikao vyake vya siku mbili kuanzia leo tarehe 10 Aprili, 2025 jijini Dodoma. 





watumishi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama la mwaka 2025, liloanza vikao vyake vya siku mbili kuanzia leo tarehe 10 Aprili, 2025 jijini Dodoma. 

   

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni