Ijumaa, 11 Aprili 2025

MKUTANO MKUU WA IAWJ WAENDELEA; MAJAJI WANAWAKE WASISITIZWA KUSIMAMIA HAKI ZA WANAWAKE

Wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) pamoja na Majaji Wanawake kutoka nchi mbalimbali duniani wanaendelea kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 17 wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (IAWJ) ulioanza  tarehe 09 Aprili, 2025.

Jana tarehe 10 Aprili, 2025 ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, mada mbalimbali zilitolewa na kusisitiza juu ya umuhimu ya Majaji na Mahakimu wanawake kusimamia haki za wanawake wanaopitia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ambapo watoa mada kadhaa wametoa uzoefu wao kuhusu namna wanavyokabiliana na vitendo hivyo.

Kaulimbiu ya Mkutano huo inasema; ‘Wanawake na uongozi katika kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ya dhidi ya wanawake.’

Wanachama wa TAWJA ni miongoni mwa jumla ya washiriki 903 wanaohudhuria katika mkutano huo wa siku nne unaotarajiwa kuhitimishwa tarehe 12 Aprili, 2025. 

Matukio katika picha ushiriki wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) unaofanyika katika Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini.                               

  



(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Cape Town)





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni