Na Fredrick Mahava- Mahakama, Sumbawanga
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe, Fredrick Manyanda amewataka watumishi
wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga kutumia na kutunza vitendea kazi vya TEHAMA
vilivyopo ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia.
Mhe.
Manyanda aliyasema hayo tarehe hivi karibuni wakati wa kikao cha watumishi
kilichofanyika katika ukumbi uliopo Mahakama Kuu Sumbawanga alipokuwa akifungua
kikao hicho cha siku moja.
“Tuwe na utamaduni wa
kuwa na vikao vya mara kwa mara kwani vikao vinasaidia kutatua changamoto zetu
kwa umoja, pia tuwe wabunifu, tujiongeze pale tunapokuwa na changamoto na tufanye
kazi kwa bidi.
Aidha, Mwenyekiti wa
Kikao hicho Mhe. Manyanda aliongeza kuwa, katika zama za teknolojia ni vizuri
vitendea kazi vya TEHAMA viendane na Mifumo ya TEHAMA iliyopo mahakamani hivyo
ni wajibu wa kila mtumishi kutumia na kutunza vitendea kazi hivyo.
Kwa upande wake, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya
Sumbawanga Mhe. Joseph Luambano alihimiza kila mtumishi kutimiza wajibu wake
kwa kuzingatia miongozo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi.
Naye, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu
E. Essaba alisema Mahakama inaendelea kutatua changamoto mbalimbali za
watumishi ikiwemo kulipa shahiki mbalimbali za watumishi kama vile nauli za
likizo na pia kuwapeleka watumishi wa Kada mbalimbali kuhudhulia semina, mafuzo
na makongamano mbalimbali yanayotekea ili kuwajengea uwezo.
Kikao hicho kilihudhuriwa
na watumishi kutoka Mahakama Kuu Sumbawanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi Rukwa na
Mahakama ya Wilaya Sumbawanga.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Fredrick Manyanda akiongoza kikao hicho cha watumishi
Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Joseph Luambano akizungumza wakati wa kikao cha watumishi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni