- Juster Tibendelena Apeperusha Bendera Mita 3000
Na
EUNICE LUGIANA-Mahakama, Mwanza
Mwanariadha
wa Timu ya Mahakama ya Tanzania [Mahakama Sports], Justa Tibendelana (Atugonza)
amepeperusha vyema bendera ya Mahakama kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mbio
za mita 3000 baada ya kutumia dakika 12 kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo
kwa Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI)
yanayofanyika jijini Mwanza.
Mbio hizo
zimefanyika jana tarehe 8 Septemba, 2025 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kuwakutanisha
wanaridha kutoka idara mbalimbali.
Katika
mbio za mita 200, Mahakama Sports iliwakilishwa na Mwajabu Bwire na Yunus
Mkurukute kwa kuwa washindi wa tatu nay
a pili, mtawalia, wakati kwenye mita 100 Mahakama Sports iliwakilishwa na Leah
Ndanda na kushika nafasi ya tatu na katika Mita 400 mwakilishi Edger Maiko
Mtimba alishika nafasi ya kwanza.
Katika
mbio za kupokezana vijiti (relay), Timu ya Mahakama Wanawake ilifanikwa kushika
nafasi ya kwanza na Wanaume nafasi ya pili.
Kutokana
na matokeo hayo, Mahakama Sports imefanikiwa kuingia fainali katika mashindano
mbio kwa mita 100, 200, 400 na mbio za kupokezana vijiti.
Wakati huo huo, Timu za Kamba Wanawake na Wanaume zimefanikiwa kuingia robo fainali ambapo upande wa Wanawake wamevuta na Timu kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu na kufanikiwa kuwavuta mivuto yote miwili na kwa upande wa Wanaume ikavutana na Ofisi ya Mashtaka na kufanikiwa kuwavuta.
Mkimbiaji
wa mita 3,000, Justa Tibendelana, maarufu Atugonza akikimbia katika mshindano
hayo.
Timu ya Ridha
Wanawake na Wanaume ya Mahakama katika picha ya pamoja kabla ya kuanza
mashindano.
Sehemu ya
wachezaji wa Timu ya Kamba Wanawake wakijiandaa kukabiliana na timu kutoka Ofisi
ya Wakili Mkuu (hawapo pichani).
Sehemu ya
wachezaji wa Timu ya Kamba Wanaume wakijiandaa kukabiliana na timu kutoka Ofisi
ya Mashtaka.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni