Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 29 Oktoba, 2025 ameungana na Watanzania wengine nchini kutimiza haki yake ya Kikatiba kwa kushiriki katika zoezi la upigaji kura wa Rais, Wabunge na Madiwani katika Kituo cha kupigia Kura cha Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma.
Mhe.
Masaju aliwasili katika viwanja vya Kituo hicho majira ya Saa 2 Asubuhi na
kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambaye pia ni Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk.
Yafuatayo
ni matukio katika picha, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju
akishiriki katika zoezi la Upigaji kura leo tarehe 29 Oktoba, 2025.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akidumbukiza karatasi ya kupigia kura mara baada ya kushiriki katika zoezi la upigaji kura leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kushoto) akifurahia jambo na na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk mara baada ya kukamilisha zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma leo tarehe 29 Oktoba, 2025.









Hakuna maoni:
Chapisha Maoni