Na. Innocent Kansha na Halima Mnete, Mahakama
Mahakama
ya Tanzania Makao Makuu na Mahakama ya Rufani jijini Dodoma tarehe 25 Oktoba,
2025 walifanya hafla ya kuwaaga watumishi wastaafu wa Mahakama ikiwa ni ishara
ya kuwaenza watumishi hao kwa utumishi wao uliotukuka na kuwapongeza kwa
jitihada zao za kuitumikia Serikali kwa kipindi chote cha utumishi wao.
Akinzungumza
katika hafla hiyo Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bw. Victor Kategere alisema Mahakama
ya Rufani ilikuwa na watumishi waliostaafu ambao walikuwa awajaagwa na Taasisi
rasmi hivyo napenda kuwapongeza kwa utumishi wao kupitia hafla hii maalumu.
“Baada
ya kukaa na kutafakari tumeona siku hii ya leo ni nzuri ili tuweze kuwaaaga
wenzetu. Lakini tu nitoe historia ndogo kwamba mwaka jana kama mwezi wa 10
Viongozi wa madereva waliniambia tunataka kuwaaga madereva wenzetu ambao
wamestaafu na bahati nzuri walikuwa wameshajiandaa ili niliwaomba wahairishe
tujipange ili tuweze kulitekeleza kwa pamoja kwa muda utakao kuwa muafaka na
leo tumeweza kulifanikisha kwa pamoja,” alisema Mtendaji wa Mahakama ya Rufani.
Mtendaji
huyo ameongeza kuwa hafla hiyo ina lengo la kutambua mchango wa tatumishi hao
wastaafu ambao kwa kipindi chote walikuwa waadilifu na wachakazi ambao
walitumikia Mahakama, Umma, Serikali na Taifa kwa ujumla kwa zaidi ya miaka 30.
“Sasa
tukio lenyewe ndo hili imefika muda wenyewe wa kuwaaga rasmi wenzetu
itakumbukwa kwamba si madereva pekee nathani kuna watumishi wengine waliostaafu
katika kipindi hicho ambao baadae watatambushwa ili tuwaone,” aliongeza
Mtendaji.
Aidha,
hafla hiyo ilitumika kuwakaribisha pia watumishi wa Mahakama ya Rufani
walihamia Makao Makuu ya Mahakama na Rufani jijini Dodoma ikiwa ni ishara ya
kuwakaribisha na kuwapongeza watumishi wote waliojaliwa kuhamia Dodoma kutoka
Dar es salaam, mikoa mingine na Taasisi zingine.
Akito neno kwa niaba ya watumishi
waliostaafu Mwandishi Mwendesha Ofisi Bi. Mameltha Simon Lumelezi alisema, mioyo
yao inafuraha ya kupindukia kama wastaafu tuliolitumikia Taifa kwa uadilifu mkubwa
sana hadi kufika hatua hii.
“Mimi nimetumika kwa miaka 35, nawaasa
watumishi waendelee kuchapa kazi mpaka Mungu atakapowafikisha kama hapa tulipofika
ni furaha sana kumaliza utumishi. Shukrani zingine ziwaendee viongozi wetu
Mtendaji Mkuu, Wasajili, Majaji ambao hawapo hapa na watumishi wenzetu na
watumishi wa Mahakama ya Rufani na Mahakama nyingine kwa sababu wengine
tumeanzia mahakama mbali mbali. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu mzuri mliokuwa
mnatuonyesha wakati tuko kazini na kutuita kuja kutuaga,” alisema Bi. Mameltha.
Wastaafu hao walioagwa katika hafla hiyo walikuwa ni Bw. Innocent Mgecha Dereva Mwandamizi, Bi. Siamini S. Magenge Msaidizi wa Ofisi, Bi. Joyce Shemdoe Mwandishi Mwendesha Ofisi, Bw. Samaidi Titi Sungu Msaidizi wa Ofisi, Bw. Romwald Dereva Mwandamizi, Bw. Joseph Chengula Dereva Mwandamizi, Bw. Thomas Mbwilo Dereva Mwandamizi, Bw. Donald Mwachisu Dereva Mwandamizi, Bw. Goha Muhoja Dereva Mwandamizi na Bw. Lema.
Watumishi Wastaafu wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bw. Victor Kategere na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Mhe. Emmanuel Mrangu wakati wa hafla ya kuwaaga.
Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bw. Victor Kategere akitoa neno la kuwakaribisha washiriki wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wastaafu.
Sehemu ya watumishi wa Mahakama ya Rufani walioshiriki kwenye hafla ya kuwaaga watumishi wastaafu.
Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bw. Victor Kategere akitoa neno la shukurani kwa washiriki wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wastaafu, kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Mhe. Emmanuel Mrangu.
Watumishi Wastaafu wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Bw. Victor Kategere na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Mhe. Emmanuel Mrangu wakati wa hafla ya kuwaaga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni