TANZIA
Marehemu Patrick Michael Masenge enzi za Uhai wake.
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Patrick Michael Masenge mwenye
cheki namba 113357034 aliyekuwa ameajiriwa kwa nafasi ya Hakimu Mkazi II
Mahakama ya Mwanzo Bunda Mjini.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Musoma Bw. Leonard John Maufi, marehemu Patrick amefikwa na umauti tarehe 10.
Oktoba, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alipokuwa amelazwa akipatiwa
matibabu. Marehemu Patrick aliajiliwa na Mahakama mnamo tarehe 28 Mwezi wa 10
Mwaka, 2024
Taratibu
za mazishi zinaendelea kuratibiwa na Mahakama kwa kushirikiana na familia.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA
LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni