Na DOTTO NKAJA-Mahakama, Geita.
Kampuni ya Parik Limited Moshi Tanzania imekamilisha
mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Ng’anzo iliyopo Wilaya ya
Bukombe mkoani Geita ulioanza tarehe 27 Julai 2024.
Jengo la Mahakama hiyo lilikabidhiwa tarehe 10 Octoba,
2025 kwa Mahakama Kuu Kanda ya Geita ili lianze kutumika.
Mhandisi Mshauri, Venjislous Mgeni kutoka Kampuni ya
Norman and Dawbarn alikabidhi jengo pamoja na rasilimali zilizopo kwa Kaimu
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Geita, Bi. Happiness Mushi.
Zoezi hilo lilishuhudiwa na Mhandisi Aika Kileo kutoka
Makao Makuu ya Mahakama, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Geita, Mhe.
Fredrick Lukuna na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Bukombe, Mhe. Zawald Nyekelela.
Wengine ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Ng’anzo, Vitus Mfumya Ofisa Utumishi wa Mahakama ya Wilaya Bukombe, Bw. Hafidhi Mtunzi na watumishi wengine kutoka Mahakama ya Wilaya Bukombe.
Kampini ya Parik Limited ikiwakilishwa na Mhandisi Joseph
Baleke ambaye alikabidhi funguo na ramani ya jengo hilo kwa Bi. Mushi.
Naye Mhe. Lukuna baada ya kushuhudia makabidhiano hayo alisema, “Kazi iliyobaki ni kungoja kibali cha ufunguzi wa jengo hili. Zoezi hilo linaratibiwa na Ofisi ya Jaji Mfawidhi.”
Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Fredrick Lukuna [wa kwanza kulia] akiwa na Kaimu Mtendaji wa Mahakama Geita , Bi. Happiness Mushi [katikati] na Mhandisi kutoka Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Bi. Aika Kileo ndani ya jengo hilo.
Timu ya makabidhiano ikifanya tathmini sehemu ya kupanda miti siku ya uzindizi wa Mahakama hiyo.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni