TANZIA
Marehemu Fredrick Binamungu Kakurwa enzi za uhai wake.
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake
wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Mwanza Mhe.
Fredrick Binamungu Kakurwa aliyekuwa
ameajiriwa kwa nafasi ya Hakimu Mkazi II akihudumu Mahakama ya Mwanzo
Nyancheche iliyopo wilaya ya Sengerema.
Kifo hicho kilitokea mnamo
tarehe 10 Oktoba,
2025 majira ya saa nne usiku eneo la Kiseke wilaya ya Ilemela akielekea
nyumbani, akitokea kazini kwake Mahakama ya Mwanzo Nyancheche iliyopo wilaya ya
Sengerema
Kwa
mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda
ya Mwanza, Bw.
Tutubi Mangazeni, marehemu Bw Fredrick Binamungu Kakurwa alifikwa na umauti
kutokana na ajali ya pikipiki iliyotokea eneo la kiseke.
Marehemu
Fredrick aliajiriwa mnamo
tarehe 28 Novemba, 2024 kama
Hakimu Mkazi II na kupangiwa kituo cha kazi Mahakama ya mwanzo Nyancheche
ambako amehudumu mpaka umauti ulipomfika.
Wakati
wa ajira yake marehemu alikuwa na elimu ya shahada ya sheria na Astashahada ya
mafunzo ya sheria kwa vitendo kutoka Chuo
cha Sheria Tanzania (Law
school of Tanzania).
Marehemu
Fredrick anatarajiwa kuzikwa
mnamo tarehe 14 Octoba, 2025 nyumbani kwao, kijiji cha Bundaza, kata ya Nyakibimbili
mkoani Kagera.
BWANA ALITOA NA BWANA
AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni