Na. Ally A. Ramadhani – Mahakama Katavi
Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Bi Jamila
Yusufu Kimaro jana tarehe 2 Februari, 2026 alikuwa Mgeni Maalumu
akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mlindoko na kuhutubia
katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini na kuipongeza Mahakama kwa kuanzisha
miradi mbalimbali ya ujenzi na miundo mbinu ya Mahakama inayoendelea Mkoani
Katavi.
Mhe. Bi. Kimaro aliitaja miradi mbalimbali
inyoendelea mkoani Katavimfano, Vituo vya Mahakama za Mwanzo kama vile Mamba,
Sibwesa, Ugalla na Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Katavi ambavyo kwa
wastani ujenzi unaendelea kukamilika.
Aidha,
Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda alisema “kukamilika kwa miradi yote ya ujenzi wa
Mahakama inayoendelea mkoani Katavi itasaidia kwa kiwango kikubwa hasa kwa
upande wa gharama za wananchi kutumia umbali mrefu kutoka eneo moja kwenda jingine
akitolea mfano; kutoka Katavi kwenda Sumbawanga kwa ajili ya kusikiliza mashauri
yao yanayoendelea Mahakama Kuu, pia kupunguza mashauri ya mlundikano (Backlog)
pamoja na muda wa kumaliza mashauri kupungua”.
Kwa
upande wake, Wakili wa kujitegemea Bw. Lutende Masinde akihutubia kwa niaba ya
Mwenyekiti wa chama cha Mawakili Tanganyika Mkoa wa Katavi Bi. Sekela Amulike
aliongeza kuwa, “Kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Mchango wa
Mahakama katika Ustawi na Maendeleo ya Taifa, Mahakama inawajibu wa kulinda
Haki na Wajibu kwa wananchi, hii itasaidia kutatua migogoro miongoni mwa wananchi,
hivyo kuongeza uzalishaji kwa Taifa,” aliongeza Bw. Masinde.
Kama
ilivyo Moja ya nguzo katika Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania ni utoaji haki
kwa wakati. Mahakama inatekeleza mpango huo kwa kuboresha mazingira ya utoaji
haki na kusogeza huduma za utoaji haki karibu zaidi na wananchi kwa kujenga
miundombinu bora na wezeshi itakayochangia ufanisi mzuri wa utekelezaji wa nguzo
hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Bi Jamila Yusufu Kimaro, ambaye ni Mgeni Maalum kwenye Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini 2026 alipokuwa akiwahutubia wananchi na wadau mbalimbali wa Mahakama mkoani Katavi.
Sehemu ya Watumishi wa Mahakama mkoani Katavi wakitoa burudani kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini
Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu
Mkazi Katavi Mhe. Gway K. Sumaye na Mgeni Rasmi wa Sherehe za Maadhimishi ya
Siku ya Sheria nchini akitoa hotuba ya siku hiyo.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni