Ijumaa, 13 Februari 2026

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA


TANZIA

Bi. Happiness Amos Majule enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. Happiness Amos Majule, aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Mahakama ya Wilaya ya Meatu.

Kifo hicho kilichotokea mnamo tarehe 09 Februari, 2026 siku ya Jumatatu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Marehemu Bi.happiness A. Majule alizaliwa tarehe 11 April, 1969 na aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe 04 Juni 1992 katika nafasi ya Msaidizi wa Ofisi.

Hadi umauti unamkuta, Bi happiness alikuwa akihudumu katika Mahakama ya Mwanzo Kisesa.

Aidha, Bi. Happyness Amos Majule anatarajiwa kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele mnamo tarehe 13 Februari, 2026 huko mkoani Singida Wilaya ya Iramba Kijiji cha Ulemo.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni