Jumatano, 18 Februari 2026

WEKEZENI KWENYE WATAALAMU NA MIUNDOMBINU YA TEHAMA: PROF. OLE GABRIEL

 Na Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama, Arusha

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel  amewashauri wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Mashirika ya Umma kuwekeza kwenye Wataalamu na Miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi.

Akiwasilisha Mada kuhusu Mifumo ya Kielekitroniki ya Ubadilishanaji wa Taarifa kwa kutumia Akili Unde kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha, Prof. Ole Gabriel alisema kuwekeza kwenye Utaalam na miundombinu ya TEHAMA kutazisaidia Taasisi na Mashirika ya Umma kuongeza tija na ufanisi.

Prof. Ole Gabriel alisema kuwa  Mahakama ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika  matumizi ya mifumo mbalimbali ya Kielekitroniki ambayo imerahisisha kwa kiasi kikubwa shughuli za utoaji haki nchini na kutoa muda kwa wananchi kushiriki katika shughuli za kujiongezea kipato.

”Taasisi inapojikita kwenye matumizi ya mifumo ya Kielekitroniki husaidia kuokoa muda kwa kuwa wananchi watapatiwa huduma kwa haraka na kwenda kufanya shughuli za uzalishaji”, alisisitiza Mtendaji Mkuu.

Mkutano wa Sita wa mwaka wa Serikali Mtandao unafanyika jijini Arusha ambapo umewakutanisha Wataalam wa masuala ya TEHAMA na wataalamu wengine zaidi ya 1,000 kutoka Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma ili unajadili  jitihada za Serikali Mtandao, mafanikio pamoja na changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa jitihada hizo na namna ya kukabiliana nazo.

Aidha. Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kumalizika kesho tarehe 19 Februari, 2026. 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha Mada kuhusu Mifumo ya Kielekitroniki ya Ubadilishanaji wa Taarifa kwa kutumia Akili Unde kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha,   
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha.   
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akitoa ufafanuzi wa hoja wakati wa Majadiliano mara baada ya kuwasilisha Mada kuhusu Mifumo ya Kielekitroniki ya Ubadilishanaji wa Taarifa kwa kutumia Akili Unde kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha.   
Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (Ajira) Bi. Enziel Mtei (wa kwanza kulia) akiwa kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha.   
Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (Maadili na Nidhamu) Bi. Alesia Mbuya (katikati) akiwa kwenye Mkutano wa Sita wa Mwaka wa Serikali Mtandao leo tarehe 18 Februari, 2026 jijini Arusha.   




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni