Mhe. Asajile Joshua Mhando enzi za uhai wake.
Kaimu Jaji Mfawidhi
Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, Mhe. Stephen M. Magoiga, anasikitika kutangaza kifo
cha Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Mwanzo Mikese, Mhe. Asajile Joshua Mhando,
aliyefariki Dunia tarehe 17 Februari, 2026 saa 7.00 mchana katika Hospitali ya
Platnum mjini Morogoro alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujisikia vibaya
akiwa kazini.
Taratibu za mazishi
zinaendelea kuratibiwa, na mara baada ya kukamilika zitatolewa.
Uongozi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Morogoro unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi
wote kwa msiba huu mzito.
Bwana alitoa, Bwana
ametwaa jina lake lihimidiwe.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni