Na. Ally Ramadhani – Mahakama, Katavi
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Mhe. Fredrick Kapela
Manyanda tarehe 27 Machi, 2026 alikabidhi rasmi eneo jipya la kiutawala la masjala
ndogo ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Katavi kwa Jaji Mfawidhi wa Kanda
hiyo Mhe. Godfrey Ntemi Isaya, katika hafla iliyofanyika katika Jengo la
Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi.
Aidha,
Mhe. Manyanda alifanikiwa kutembelea jengo jipya la Kituo Jumuishi cha Utoaji
Haki (IJC) Katavi na kufanya ukaguzi wa vifaa vya ofisi kisha kufanya makabidhiano
kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Katavi Mhe. Godfrey Ntemi
Isaya.
Baada
ukaguzi huo Mhe. Manyanda alifanya kikao cha kuagana na watumishi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania Masjala ndogo Katavi na kuwashukuru kwa ushiriakiano alioupata
kutoka kwao na kuahidi kuwa ataendelea kutoa ushirikiano wakati wote atakapo
hitajika. Vilevile, aliwakumbusha umuhimu wa kuendelea kutoa huduma bora kwa
wananchi.
“Kabla
ya mwaka 2005, wakazi wa Sumbawanga na Katavi walikua wanapata Huduma za
Mahakama Kuu kutoka Kanda ya Mbeya ila mwaka 2005 nasi tukapata Huduma za
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga na leo hii mwaka 2026 nina furaha kubwa sana
kuwa kwenye historia ya tukio hili la kukabidhi eneo jipya la kiutawala la
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo Katavi,” alisema Mhe. Manyanda.
Kwa
upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Katavi Mhe. Godfrey
Ntemi Isaya, aliwasisitiza watumishi kuhusu suala la nidhamu, kuthaminiana,
upendo, ulinzi wa miundombinu, vitendea kazi wa vya Ofisi na utendaji wa kazi
mzuri kwa watumishi wote ili kuwezesha kutoa huduma bora ya haki kwa wananchi.
Vilevile,
Mhe. Isaya ameupongeza Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji haki kwa kusogeza huduma za
utoaji haki kwa wananchi kwa kujenga miundombinu bora na wezeshi itakayochangia
ufanisi mzuri.
Kufuatia
makabidhiano hayo, Mhe. Manyanda aliambatana na Naibu Msajili Mahakama Kuu
Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Pamela S. Mazengo pamoja na Kaimu Mtendaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Bi. Irene Mlangwa.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Mhe. Fredrick Kapela
Manyanda (Katikati) akimkabidhi Hati ya makabidhiano Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Katavi Mhe. Godfrey Ntemi Isaya (kushoto) kuashiria shughuli rasmi
za Mahakama Kuu, Kanda ya Katavi.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Kanda ya Katavi Mhe. Godfrey
Ntemi Isaya (wa kwanza kushoto) akionesha hati ya makabidhiano.
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Thadeo M. Mwenempazi (wa Kwanza
Kushoto) akikabidhi zawadi kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda
ya Sumbawanga Mhe Fredrick Kapela
Manyanda (wa Kwanza Kulia), iliyo andaliwa na Uongoz wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Masjala ndogo ya Katavi.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Mhe. Fredrick Kapela
Manyanda akionesha tuzo (Troph) aliyozawadia na Uongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Masjala ndogo ya Katavi kupitia Mhe Thadeo M. Mwenempazi Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania
kanda ya Sumbawanga.
Naibu
Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Pamela S. Mazengo akilishwa keki
na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Katavi Mhe.
Godfrey Ntemi Isaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni