Na NOEL SYLIVESTER – Mahakama, Songea
Menejimenti
ya Mahakama, Kanda ya Songea, tarehe 26
Machi 2026 ilifanya kikao cha tathmini ya utendaji
kazi kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Kikao
hicho kilifanyika katika ukumbi wa Saint Vicent, wilayani Nyasa na kilifunguliwa rasmi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho.
Katika
kikao hicho, taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mahakama kwa kipindi cha
Januari hadi Machi, 2026
iliwasilishwa na Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Songea, Bw. Allan Mwela, ambaye
alihudumu pia kama Katibu wa kikao.
Akiwasilisha
taarifa hiyo, Bw. Mwela alieleza masuala mbalimbali ikiwemo utawala bora,
uwajibikaji pamoja na usimamizi wa rasilimali. Aligusia pia nguzo ya kwanza
inayohusu utawala na usimamizi wa uendeshaji wa shughuli za Mahakama.
Naye Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya
Songea, Mhe. Lilian Rugalabamu,
aliwasilisha taarifa inayohusu utoaji wa haki kwa wakati ambayo iligusia
masuala ya usimamizi wa mashauri na usimamizi wa mashauri kwa njia ya mtandao
(VC).
Kwa upande mwingine, Afisa Rasilimaliwatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Bi. Paulina Kapinga, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mahakama kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2026.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha.
Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Lilian Rugalabamu.
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Songea, Bw. Allan Mwela.
Afisa rasilimaliwatu, Bi.Paulina Kapinga (aliyesimama).
Habari hii imehaririwa na FAUSTNE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni