Na. IMAN PATSON – Mahakama, Songwe
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga jana
tarehe 25 Machi, 2026 alikabidhi rasmi eneo jipya la kiutawala la Mahakama Kuu
Masjala Ndogo Kanda ya Songwe kwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo Mhe. Gabriel
Malata, katika hafla iliyofanyika katika Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Songwe.
Aidha,
Mhe. Tiganga alifanya ukaguzi wa jengo hilo jipya ambapo alipitia miundombinu
ya jengo na vifaa vya Ofisi na kisha kufanya makabidhi kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu, Kanda ya Songwe Mhe. Malata.
Mhe.
Tiganga alipongeza wakandarasi wa Jengo hilo kwa kazi nzuri waliofanya na pia
aliwasihi wafanyakazi wa jengo hilo kumalizia kazi iliyobakia kwa muda mfupi
ili kazi zingine za kimahakama ziweze kuendelea.
Aidha,
baada ukaguzi huo Mhe, Tiganga alifanya kikao cha kuagana na watumishi wa
Mahakama Kanda ya Songwe na kuwashukuru kwa ushiriakiano alioupata kutoka kwao
na aliwaahidi kuwa ataendelea kutoa ushirikiano wakati wote atakapo hitajika. Vilevile,
aliwakumbusha umuhimu wa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kwa
upande wake, Jaji Mfawidhi Mhe. Malata aliwasisitiza watumishi kuhusu suala la
nidhamu, kuthaminiana, upendo, ulinzi wa miundombinu, vitendea kazi wa vya Ofisi
na utendaji wa kazi mzuri kwa watumishi wote ili kuwezesha kutoa huduma bora ya
haki kwa wananchi.
Mhe.
Malata Uongozi wa Mahakama kwa kumteua kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Songwe na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha haki
inatolewa kwa wananchi kwa wakati mapema ipasavyo.
Kufuatia
makabidhiano hayo, Mhe. Tiganga aliambatana na Naibu Msajili Mahakama Kuu, Kanda
ya Mbeya Mhe. Aziza Temu pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi.
Mavis Miti.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga
(kulia) akifanya makabidhiano na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songwe Mhe.
Gabriel Malata (kushoto) kuashiria shughuli rasmi za Mahakama Kuu, Kanda ya
Songwe.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo Kanda ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa kwanza
kushoto) akionesha hati ya makabidhiano.
Muonekano
wa Jengo la Mahakama Kuu Masjala Ndogo Kanda ya Songwe lilipofikia.
Mhandisi
wa jengo jipya la Kituo Jumuishi cha Utoaji haki Kanda Songwe Bw. Victor akielezea
maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo lilipofikia na akiahidi kuwa kufikia Aprili
1, 2026 jengo hilo litakua lipo tayari kwa matumizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni