Alhamisi, 26 Machi 2026

JAJI MFAWIDHI MBEYA AFUNGUA MAFUNZO YA USULUHISHI KWA NAIBU WASAJILI, MAHAKIMU WAKAZI

Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga amefungua mafunzo maalum ya Usihi na Usuluhishi kwa Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi kutoka katika Kanda mbalimbali za Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Iringa, Njombe, Sumbawanga, Songwe na Katavi.

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa tarehe 24 Machi, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya. Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhe. Tiganga alisema kuwa usuluhishi unalenga kuimarisha upatikananaji wa haki mapema ipasavyo na kwa gharama nafuu.

“Usuluhishi ni nguzo muhimu sana katika utoaji haki, kwani hupunguza migogoro baina ya wanajamii na kupunguza gharama kwa wadaawa katika kutatua migogoro yao,” alisema Mhe. Tiganga.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Gloria Shuma akizungumza na washiriki alisema kuwa, mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu yana lengo mahususi la kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani na kupunguza athari za upatikanaji wa vidonda na makovu ambayo ni matokeo ya migogoro katika jamii.

Aidha, washiriki walieleza kuwa matarajio yao katika mafunzo hayo ni kujifunza kwa kubadilishana uzoefu baina yao namna ya kufanya usihi na usuluhishi, kujifunza namna ya kuwa wasuluhishi bora na kubaini changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa usuluhishi na namna ya kuzitatua kwa pamoja.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2013, Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania pamoja na sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya mwaka 2019.

    Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waheshimiwa Naibu Wasajili na Waheshimiwa Mahakimu Wakazi kutoka katika Kanda mbalimbali za Nyanda za Juu Kusini wanaoshiriki mafunzo hayo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi ambao ni Naibu Wasajili wanaoshiriki Mafunzo ya Usuluhishi kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Sehemu ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia mada zinazotolewa na wawezeshaji kwenye mafunzo hayo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga (aliyesimama kwenye podium) akifungua mafunzo hayo maalum kwa Waheshimiwa Naibu Wasajili na Waheshimiwa Mahakimu Wakazi.

Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu (kushoto) akiwa sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo

Sehemu ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia mada zinazotolewa na wawezeshaji kwenye mafunzo hayo.

Sehemu ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia mada zinazotolewa na wawezeshaji kwenye mafunzo hayo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Momba ambaye pia ni mwezeshaji Mhe. Raymond Kaswaga akitoa mada kwenye mafunzo hayo ya Usuluhishi

Sehemu ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia mada zinazotolewa na wawezeshaji kwenye mafunzo hayo.

Mratibu wa mafunzo hayo Mhe. Gloria Shuma (kulia) kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) akifuatilia mafunzo hayo, kushoto ni Hakimu Mkazi Mahakama Kuu Mbeya Mhe. Franco Msuja

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni