- Watumia jukwaa hilo kutoa elimu ya sheria kwa umma
- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo awapongeza
Na
PAUL MUSHI- Mahakama, Moshi
Wanachama
wa Chama cha Majaji na Mahakimu (TMJA) Tawi la Kilimanajaro, wakiongozwa na
Mlezi wao, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, Mhe. Dkt.
Lilian Mongella, hivi karibuni walishiriki kikamilifu kwenye mbio za urefu wa
Kilomita 42, 21 na 5 katika kwenye tamasha kubwa la michezo la International
Kilimanjaro Marathon.
Tamasha
hilo lililofanyika kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 22 Machi, 2026 liliongozwa na Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda na kushirikisha Wadau wa
michezo wa ndani ya nchi na mataifa mbalimbali duniani. Mhe. Makonda pia alitoa
zawadi kwa washindi katika mbio za aina tofauti.
Baada
ya kutoa zawadi hizo, Waziri Makonda alitembelea na kukagua mabanda yaliyokuwa
yanatoa huduma mbalimbali, likiwemo la TMJA lililokuwa linatoa elimu ya masuala
ya kisheria kwa Wananchi.
Akiwa
kwenye banda hilo, Mhe. Makonda aliwapongeza Majaji na Mahakimu kwa kutumia jukwaa hilo kuimarisha afya zao
na kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria.
“Nilipata
taarifa ya uwepo wenu katika tamasha hili, kwakweli sikutegemea kama mngekuwepo.
Nawapongeza sana kwa kazi kubwa mliyoifanya, hasa ya kutoa elimu katika siku
hizi zote toka siku ya ufunguzi. Niwaombe muendelee na awamu zijazo ili
muwafikie watu wengi zaidi kwa elimu hii mnayotoa,” alisema Waziri Makonda.
Naye
Mhe. Dkt. Mongella aliwapongeza washiriki kwa kujitoa kwao katika hali na mali
kushiriki katika tamasha hilo kwa lengo la kuimarisha afya zao na kutoa elimu
kwa watu wenye uhitaji kwenye masuala ya kisheria.
“Nawapongeza
sana viongozi wa Tawi letu la TMJA Kilimanjaro kwa kuona umuhimu kwa kushiriki
tamasha hili kubwa. Hili si tu kwamba ni muhimu katika kujenga afya zetu, bali
pia jambo la kutoa elimu ni kubwa zaidi, hasa kwa kuzingatia uwingi wa watu
katika tamasha,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Rais wa TMJA, Mhe, Elimo Massawe, aliyeambatana na Katibu wa
Chama hicho, alipata fursa ya kutembelea na kuona shughuli zilizofanyika wakati
wa tamasha hilo.
Mhe. Masawe naye aliwapongeza wanachama wa Tawi hilo kwa kazi kubwa waliyofanya na kuwapa shime ya kuendelea kuwa wabunifu na kufanya zaidi kwa siku zijazo.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, Mhe. Dkt. Lilian Mongella
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la maonyesho katika
viwanja vya ushirika Moshi yalipofanyikia mashindano ya Kilimanjaro Marathon
2026.
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, (wa kwanza kushoto mwenye
fulana ya njano) akikabidhiwa zawadi na Mjumbe wa Baraza Tendaji Taifa wa Chama
cha Majaji na Mahakimu, Mhe. James Kapele, kwa niaba ya mlezi wa Tawi, baada ya
kutembelea banda la chama hicho.
Watumishi
wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi wakitoa elimu kwa Wananchi waliofika katika
banda la Mahakama katika viwanja vya ushirika Moshi yalipofanyikia mashindano
ya Kill Marathon 2026.
Rais
wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Mhe. Elimo Massawe, alipotembelea
banda la TMJA Tawi la Kilimanjaro wakati wa tamasha la Kilimanjaro Marathon
2026.
Baadhi
ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki mbio wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya kumaliza mbio za Kill marathon 2026.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Arusha.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni