Jumanne, 24 Machi 2026

MBEYA YAZINDUA MAHAKAMA TATU ZA MWANZO

Na MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga ameongoza hafla ya uzinduzi wa Majengo Mapya Matatu (3) ya Mahakama za Mwanzo. Majengo hayo matatu yaliyozinduliwa ni pamoja na Mahakama ya Mwanzo Lupatingatinga wilayani Chunya, Mahakama ya Mwanzo Ndobo Wilaya ya Kyela na Mahakama ya Mwanzo Madibila Wilaya ya Mbarali.

Hafla hiyo ilifanyika tarehe 23 Machi, 2026 katika Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Lupatingatinga wilayani Chunya. Uzinduzi wa Mahakama hizo unalenga kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi, kupunguza umbali wa kufuata huduma za kimahakama na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki kwa wakati mapema ipasavyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Tiganga, aligusia dhima ya Mahakama katika kutoa haki kwa wakati unaostahili bila kuchelewesha huduma hizo za msingi kwa wananchi.

“Haki ndiyo msingi wa ustawi wa amani na usalama wa wananchi, na sisi kama Mahakama tumejidhatiti katika utoaji wa haki kwa watu wote na tuko tayari kufanya hivyo mapema ipasavyo,” alisema Mhe. Tiganga.

Vilevile, Mhe. Tiganga aliwaasa watumishi wa Mahakama katika Vituo hivyo kuhakikisha huduma zitakazotolewa zinaakisi hadhi ya Majengo hayo, na kusisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa haki na weledi kwa kuzingatia uadilifu na misingi ya utumishi wa umma.

Aidha, aliuomba uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kusaidia upatikanaji wa viwanja katika kila kata ili kufikia lengo la Mahakama ya Tanzania la kusogeza huduma za Mahakama karibu zaidi na wananchi.

Kwa upande wake, mgeni maalum katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Alhaj Baraka Batenga, aliwaasa wananchi kuyatunza na kuyahifadhi Majengo hayo kwani ni kwa ajili ya kulinda msingi wa amani na kudumisha ustawi wa utoaji haki kwa wananchi.

“Mahakama ni mali ya wananchi, hivyo ni wajibu wetu sote kuyalinda na kuyatunza majengo ya Mahakama zetu pamoja na miundombinu yake kwa ujumla,” alisema Mhe. Batenga.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Kasaka, alitoa shukrani kwa Mahakama ya Tanzania kwa kuwezesha kukamilika kwa Majengo hayo ya kisasa, ambayo yatasogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi.

“Suala la utoaji haki kwa wananchi mapema ipasavyo linaendana sambamba na ukaribu wa upatikanaji wa huduma za kimahakama,” alisema Mhe. Kasaka.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu, Kanda za Mbeya na Songwe, akiwemo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Songwe, Mhe. Gabriel Malata, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Mussa Pomo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu na Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo Songwe Mhe. Joyce Minde.

Wengine ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bi. Mavis Miti, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Songwe Bw. Sostenes Mayoka na Mahakimu Wakazi wakiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer.

Aidha, Uongozi wa Wilaya ya Chunya uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Alhaj Baraka Batenga, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Kasaka na viongozi wengine.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Majengo Mapya Matatu (3) ya Mahakama za Mwanzo za Lupatingatinga wilayani Chunya, Mahakama ya Mwanzo Ndobo Wilaya ya Kyela na Mahakama ya Mwanzo Madibila Wilaya ya Mbarali, tarehe 23 Machi, 2026 katika Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Lupatingatinga wilayani Chunya.

Sehemu ya wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo.

Sehemu ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya na Mkoa wa Mbeya waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi waliosimama mbele wakiongoza na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya Mbeya Mhe. Tedy Mlimba (watatu kulia)


Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka (kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa pili kulia), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Alhaj Baraka Batenga (wa pili kushoto).




Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla hiyo, wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka (kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa pili kulia), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Alhaj Baraka Batenga (wa pili kushoto).

Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama waliohudhuria hafla hiyo, wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka (kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa pili kulia), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Alhaj Baraka Batenga (wa pili kushoto).

Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama waliohudhuria hafla hiyo, wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka (kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa pili kulia), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Alhaj Baraka Batenga (wa pili kushoto).
Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya Mkoa wa Mbeya waliohudhuria hafla hiyo, wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka (kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Songwe Mhe. Gabriel Malata (wa pili kulia), Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Alhaj Baraka Batenga (wa pili kushoto).

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akipanda Mti wa Matunda katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Lupatingatinga.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (kulia) akikabidhi kibao cha Ufunguzi wa Mahakama ya Mwanzo Madibila kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbarali Mhe. Emily Mwambapa.



Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (kulia) akikabidhi kibao cha Ufunguzi wa Mahakama ya Mwanzo Ndobo kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Kyela Mhe. Rosta Mofuga.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi Jengo la Mahakama ya Mwanzo Lupatingatinga pamoja na majengo mengine mawili ya Mahakama za Mwanzo Ndobo na Madibila.

Kikundi cha ngoma za asili “Dedede” wakitumbuiza katika hafla hiyo.

Sehemu ya watumishi wa Mahakama waliohudhuria katika hafla hiyo.


Sehemu ya watumishi wa Mahakama waliohudhuria katika hafla hiyo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni