Na NOEL SYLIVESTER-Mahakama, Songea
Mahakama ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa Mahakama za Mwanzo tatu,
Lilolndo, Likuyusekamaganga na Nalasi, zilizopo katika Mahakama Kuu ya
Tanzania, Kanda ya Songea, mkoani Ruvuma.
Mahakama za Mwanzo Lilondo ipo Wilaya ya Songea katika Halimashauri ya
Madaba, Mahakama ya Mwanzo Likuyusekamaganga ipo katika Wilaya ya Namtumbo na Mahakama
ya Mwanzo Nalasi ipo katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Ujenzi huo uliokuwa unatekelezwa na Mkandalasi Mkuu (Pivotech), akisaidiana
na Mkadalasi Msaidizi(Cadson) na majengo hayo matatu ya Mahakama yamegharimu jumla
ya Shilingi za Kitanzania 2,954,059,829.18.
Mahakama ya Mwanzo Lilondo imegharimu 985,625,739/=, Mahakama ya Mwanzo
Likuyusekamaganga imegharimu 961,400,162/= na Mahakama ya Mwanzo Nalasi imegharimu
1,007,033,928.18/=.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele, alikabidhiwa majengo hayo hivi karibuni kwa nyakati tofauti na Mkandarasi Arqes Africa Architects and Interior Designers Ltd.
Alitoa shukrani kwa wananchi
wa maeneo hayo kwa ushirikiano waliouonyesha tangu kuanza hadi kumalizika kwa
miradi hiyo.
Alieleza kuwa uzinduzi wa Mahakama hizo umepangwa kufanyika tarehe 10 Aprili, 2026 katika Mahakama ya Mwanzo Lilondo, kama kuashiria kuanza kwa huduma za kimahakama zitakazoanza kutolewa katika majengo hayo mapya yaliyokamilika.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Lilondo.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Likuyusekamaganga.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Nalasi.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele (wa pili kulia) akikabidhiwa hati ya jengo Mahakama ya Mwanzo Lilondo.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele (wa
katikati) akikabidhiwa hati ya jengo Mahakama ya Mwanzo Likuyusekamaganga.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele (kushoto) akikabidhiwa hati ya jengo Mahakama ya Mwanzo Nalasi.
Wananchi na wakazi wa Nalasi wakiwa katika eneo la tukio wakishuhudia makabidhiano hayo.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni