Na LIGHTNESS KABAJU-Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Morogoro
Katika kuimarisha utendaji wa Taasisi na ustawi wa Watumishi
wa Mahakama, jana tarehe 10 Aprili, 2026 wajumbe wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi
wamefanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi mjini Morogoro.
Kikao hicho kimehudhuriwa na baadhi ya Watumishi pamoja
na wajumbe wengine, akiwemo Bw. Alquine Masubo kutoka TUGHE Makao Makuu, Bw. Steven
Wadi, ambaye ni mjumbe wa TUGHE Baraza Kuu serikalini, Bw. Anthelmus Tarimo,
ambaye ni Mwakilishi wa Katibu TUGHE Mkoa na Bi. Christina Matage, ambaye ni
Afisa Kazi Mwandamizi Idara ya Kazi kwa Mkoa wa Morogoro.
Baraza
hilo limekutana katika kikao chake cha kawaida kwa kila mwaka chini ya uongozi
wa Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu Divisheni
ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, kwa
lengo la kupitia utekelezaji wa majukumu na kujadili bajeti ya mwaka wa fedha
2026/2027.
Malengo
mengine ni kufanya uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi,
kupokea na kujadili hoja za Watumishi kwa ajili ya kuziwasilisha katika Baraza Kuu
la Wafanyakazi la Mahakama ya Tanzania.
Akifungua kikao hicho, Mhe. Mlyambina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza
alisisitiza umuhimu wa wajumbe kushiriki kikamilifu katika mijadala na kutoa
michango yenye tija itakayosaidia kuimarisha ufanisi wa Taasisi. Vilevile, alieleza
kuwa Baraza la Wafanyakazi ni chombo muhimu kinachowezesha ushirikishwaji wa Watumishi
katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya Mahakama kwa ujumla.
Katika kikao hicho, Bi. Christina Matage, kwa mujibu wa sheria aliongoza
uchaguzi wa kumpata Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Mahakama Kuu Divisheni
ya Kazi, ambapo Bi. Stella Omozo, alichaguliwa kuwa Katibu, huku Bw. Godfrey
Albetus, akiwa Katibu Msaidizi.
Aidha,
Bw. Robert Mchocha alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi
katika Baraza Kuu la Wafanyakazi.
Katika
kuwashirikisha wajumbe, Bi. Joyce Mulugu, ambaye ni Mtendaji wa mMhakama Kuu Divisheni
ya Kazi aliwapitisha wajumbe katika taarifa ya utendaji kazi, huku Bw. Fredrick
Tenga, ambaye ni Afisa Hesabu Mkuu, aliwapitisha wajumbe katika kujadili bajeti
ya mwaka wa fedha 2026/2027, wakilenga kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo
zinatumika kwa ufanisi na kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa.
Aidha,
hoja mbalimbali zilizowasilishwa zilijikita katika kuboresha mazingira ya kazi,
kuongeza motisha kwa Wafanyakazi, pamoja na kuimarisha huduma zinazotolewa na Mahakama.
Sambamba na hilo, Wajumbe wa Baraza walipata fursa ya kujadili hoja za Wafanyakazi
wa mMhakama Kuu Divisheni ya Kazi zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu
yao na kupendekeza ziwasilishwe katika Baraza Kuu la Wafanyakazi.
Sambamba na hilo, wajumbe kutoka TUGHE walitoa pongezi zao kwa Jaji Mfawidhi katika kusimamia utoaji elimu kwa watumishi, pamoja na kupokea tuzo ya ubunifu, huku wakipongeza taarifa zilizowasilishwa kwa wajumbe kwani zililenga vipaumbele muhimu katika utekelezaji wa majukumu.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (katikati)
pamoja na wajumbe.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina (katikati) pamoja na wajumbe kutoka TUGHE.
Mwakilishi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi katika Baraza
Kuu la Wafanyakazi, Bw. Robert Mchocha.
Mwenyekiti akiwa na Katibu na Katibu Msaidizi waliochagulia (mbele) pamoja na Viongozi wa Baraza la Wafanyakazi waliomaliza muda wao.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe, Dkt. Yose Mlyambina (katikati) akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni