Jumatano, 22 Aprili 2026

JAJI NONGWA AANZISHA TAWI LA TAWJA MAHAKAMA NJOMBE

Na ABDALLAH SALUM, Mahakama-Njombe

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe,Mhe. Victoria Nongwa   ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ameanzisha Tawi la Chama hicho Mahakama Kuu Njombe kinachowajumuisha Mahakimu na Majaji Wanawake.

Tawi hilo limeanzishwa kupitia alichofanya Mhe. Nongwa tarehe 20 Aprili, 2026 na Mahakimu wanawake waliopo Mkoa wa Njombe pamoja na Mahakimu waliopo Wilaya za Makete, Ludewa na Wanging’ombe kwa kutumia mkutano mtandao (Video Conference).,

Aidha, Jaji Nongwa alizungumza pia na Mahakimu wanawake wa Mahakama za Mwanzo ambapo alianza kuwaambia Mahakimu hao wampendekeze Kiongozi ambaye atakuwa Mratibu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Kanda ya Njombe ambaye alipendekezwa, Mhe. Matilda Kayombo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Njombe aliyepigiwa kura nyingi

Baada ya Mhe. Kayombo kuteuliwa kuwa Mratibu wa TAWJA aliwashukuru Mahakimu wanawake wenzake kwa kupewa nafasi hiyo ya kuwa Mratibu kwa Kanda ya Njombe na kuomba ushirikiano pamoja na kuongoza vikao vyote vitakavyoendelea itakapobidi.

 Kwa upande wake, Mhe. Nongwa baada ya uchaguzi wa kumpata Mratibu wa TAWJA Njombe, aliwasisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Taasisi na Idara mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu katika Mashirika na Taasisi mbalimbali mkoani humo. 

Mahakimu wanawake wa Mahakama Kanda ya Njombe walishukuru kwa kuanzishwa kwa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tawi la Njombe na kufahamu umuhimu wa kujiunga na Chama hicho.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na  Mahakimu wanawake (TAWJA) , Mhe. Victoria Nongwa akizungumza na Mahakimu wanawake tarehe 20 Aprili, 2026 lengo likiwa ni uanzishwa wa Tawi la TAWJA Mahakama-Njombe.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Njombe, Mhe.Victoria Nongwa akiwa katika kikao na sehemu ya Mahakimu wanawake wa Mahakama Njombe. Dhumuni la kikao hicho ni kuanzisha Tawi la Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Njombe.

Sehemu ya Mahakimu Wanawake wa Mahakama Njombe walioshiriki katika kikao hicho wakimsikiliza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Njombe, Mhe. Victoria Nongwa (hayupo katika picha). Kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Njombe, Mhe. Matilda Kayombo katikati ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Njombe Mjini,  Mhe.Lisa Abel na kulia ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Njombe Mjini, Mhe. Maria Kiduge (hayupo katika picha).

  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Njombe Mjini, Mhe. Maria Kiduge akimsikiliza kwa umakini Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Njombe, Mhe. Victoria Nongwa (hayupo katika picha).


(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni