Jumanne, 28 Aprili 2026

MASHAURI 48 YA MAHAKAMA YA RUFANI KUSIKILIZWA MASJALA NDOGO MBEYA

Na. MWINGA MPOLI – Mahakama, Mbeya

Mashauri ya Rufaa 48 ya Ardhi, Kazi na Ndoa yanatarajiwa kumalizika katika kikao cha Uendeshaji wa Mashauri (session) katika Masjala Ndogo ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania mkoani Mbeya.

Kikao hicho kinachoendeshwa na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, kikiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye ambaye ameambatana na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Eliezer M. Feleshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Deo J. Nangela, wakisaidiwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Daudi P. Kinywafu pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ya Rufani.

Akiongea katika kikao cha mapokezi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mkuye aliushukuru uongozi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya unaongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim C. Tiganga kwa maandalizi na mapokezi mazuri. Alifafanua kuwa, ushirikiano kutoka kwa wadau na wahusika, utawezesha umalizaji wa mashauri hayo kama ilivyopangwa.

“Tunawashukuru sana kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya kikao hiki kwa hakika tumefarijika sana na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunaamini kuwa mashauri haya yote tutayasikiliza bila kikwazo chochote,” alisema Mhe. Mkuye.

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga ameahidi kutoa ushirikiano kwa kipindi chote ambacho Waheshimiwa hao watakuwepo Masjala Ndogo ya Mbeya kuendesha usikilizaji wa mashauri hayo ya Mahakama ya Rufani.

Kikao cha usikilizaji wa Mashauri hayo kimeanza jana tarehe 27 Aprili, 2026 na kinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 22 Mei, 2026.

Mwenyekiti wa jopo la Majaji ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye akisaini katika kitabu cha wageni mara tu baada ya kuwasili Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mbeya.

Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye wakiwa pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mbeya wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Masjala Ndogo Mbeya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa waheshimiwa Majaji hao mara baada ya kuwapokea.

Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye wakisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Pamoja na watumishi mbalimbali.

Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye wakisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Pamoja na watumishi mbalimbali.

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Daudi kinywafu (wa pili kushoto kushoto), Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mbeya Mhe. Aziza Temu (kulia), Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mbeya Mhe. Judith lyimo (wa kwanza kulia) na Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti wakishiriki mapokezi hayo.

Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye wakisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Pamoja na watumishi mbalimbali.

Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Rehema K. Mkuye wakisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Pamoja na watumishi mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni