Na. SHARIFU MOKIWA -Mahakama, Sumbawanga
Wanachama wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (Tanzania Magistrates and Judges Association (TMJA) Tawi la Rukwa walikutana hivi karibuni na kufanya kikao maalumu kilicholenga kuimalisha ushirikiano wa kitaaluma, kujadili maendeleo ya chama ili kujenga mshikamano miongoni mwa wanachama. Kikao hicho kilifanyika katika ufukwe wa Kasanga ziwa Tanganyika.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Sumbawanga, Mhe. Frederick Kapela Mayanda alisisitiza umuhimu wa umoja, ushirikiano na ushiriki wa wanachama katika kuimalisha utendaji wa Chama pamoja na utoaji wa haki kwa jamii.
Wakati wa kikao hicho Baraza Tendaji la TMJA Tawi la Rukwa lilipokea taarifa mbali mbali ikiwemo tarifa ya uimarishaji wa Tawi, taarifa ya mwakilishi wa TMJA pamoja na taarifa ya Mhazini wa Tawi ambapo wanachama walipata nafasi ya kujadili maendeleo yaliyofikiwa pamoja na changamoto zinazokikabili Chama.
Aidha, majadiliano mbali mbali yalifanyika na maazimio muhimu kutolewa kwa lengo la kuimalisha Tawi na kuboresha ushirikiano wa wanachama katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wanachama pia walipata mafunzo maalum kuhusu program ya Mentorship yaliyotolewa na Mhe. Manyanda, mafunzo hayo yalilenga kuongeza uelewa wa kitaaluma, kurejesha utendaji wa kazi pamoja na kujenga mazingira bora ya ushauri na uongozi ndani ya Taasisi.
Vilevile, baada ya kikao na mafunzo wanachama waliendelea na shughuli za utalii katika eneo la Kasanga, hatua iliyosaidia kuongeza ukaribu kujenga mahusiano bora ya kikazi pamoja na kuweka kumbukumbu nzuri za pamoja.
Kikao hicho kilihudhuliwa na na Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Sumbawanga, Mhe. Frederick
Kapela Mayanda, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Sumbawanga Mhe.
Thadeo Mwenempazi, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Sumbawanga Mhe.
Pamela Mazengo pamoja na Mahakimu wa ngazi mbali mbali.
Picha ya pamoja ya Wanachama wa Chama cha Mahakimu na Majaji
Tanzania (TMJA) Tawi la Rukwa.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Sumbawanga, Mhe. Frederick Kapela Mayanda akifungua kikao cha TMJA Tawi la Rukwa.
Wanachama wa TMJA Tawi la Rukwa wakiwa kwenye kikao
wakifatilia na kusikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zikiwasilishwa.
Mwakilishi wa TMJA Tawi la Rukwa Mhe. David Mbembela (aliyesimama) wa
Baraza la TMJA Taifa akiwasilisha taarifa wakati wa kikao
Sehemu ya Wanachama wakiwa katika Fukwe za ziwa Tanganyika ikiwa ni sehemu ya Utalii.
Mwenyekiti wa TMJA Tawi la Rukwa (kulia) akimpa mkono wa shukrani wakati wa kumuaga Mhe. Elisha Daudi Mwasomola (kushoto) ambaye amehamishiwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Njombe.
Picha ya pamoja ya Wanachama wapya na waliohamia (TMJA) Tawi la Rukwa.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni