Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Kisutu
Mradi wa Mfumo Endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania (BSAAT), hivi karibuni umekabidhi vifaa mbalimbali vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Hakimu Mkazi Mkuu na
Afisa Mwambata wa BSAAT, Mhe.
Richard Kabate, alikabidhi vifaa hivyo kwa Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Franco Kiswaga, huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bi. Athanasia Kabuyanja.
Watumishi
wengine wa Mahakama waliokuwepo wakati wa makabidiano hayo ni Ofisa
Utumishi Mwandamizi, Bw. Nkruma
Katagira, Mhasibu Mwandamizi, Bi. Prisca Gideon na Ofisa TEHAMA wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bw. Winfred Nzilano.
Vifaa
vilivyokabidhiwa ni Kompyuta Mpakato tano (5) aina ya HP Omnibook X
Flip, Begi za Kompyuta
Mpakato (Laptop bag) tano (5), Adapta (Type
C to HDTV 11 in 1 Adapter) na Vipanya
vya Kompyuta (wireless mouse) tano (5) na Vipanga
Njia (Portable router) tano (5).
Akizungumza
waakati wa zoezi hilo, Mhe. Kabate
aligusia umuhimu wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi
katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba Mahakama ya Kisutu imekuwa ikipokea
kesi nyingi ambazo zinahusiana na maswala ya rushwa.
Hivyo, alibainisha kuwa makabidhiano hayo ni
katika kuhakikisha uondoaji wa mianya ya rushwa katika mifumo ya Mahakama na kuongeza wigo wa
kushughulikia mashauri ya rushwa.
Naye Hakimu Mfawidhi aliushukuru uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kuona kwamba inafaa kuwaletea vitendea kazi. Alisema watavitumia vifaa hivyo kuhakikisha mashauli yanamalizika kwa haraka iwezekanavyo kama kauli mbiu ya Mahakama inavyosema.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni