Jumatatu, 4 Mei 2026

WANA-TAWJA KANDA YA DAR ES SALAAM WAKUTANA KIGAMBONI

Na EUNICE LUGIANA, Mahakama-Dar es Salaam

Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Kanda ya Dar es Salaam wamekutana kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kufurahi kwa pamoja sambamba na kufanya uchaguzi wa Mratibu wa Chama hicho katika Kanda hiyo.

Hafla hiyo ilifanyika tarehe 01 Mei, 2026 katika Kijiji cha Mwasonga-Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mlezi wa TAWJA Kanda ya Dar es Salaam ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi alisema kwamba, TAWJA ni yao na hawawezi kuikwepa huku akinukuu maneno ya Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Sharmillah Sarwatt aliyeomba hafla hizo zifanyike mara mbili kwa mwaka na wajumbe waliridhia na hivyo akamuomba Mhe. Sarwatt awe Muandaaji Mkuu wa shughuli hizo.

Wakati wa mtoko huo, Mhe. Maghimbi alimteua Mhe. Zenas Tarimo kutoka Mahakama ya Mwanzo Ilala kuwa Mratibu wa sherehe zote za TAWJA na Mhe. Irene Maganga kutoka Mahakama ya Mwanzo Kimara kuwa Mratibu Msaidizi wa sherehe.

Akizungumza baada ya uteuzi huo, Mhe. Tarimo amewaomba WanaTAWJA wa Kanda ya Dar es Salaam kumuunga mkono ili kumuwezesha kufanya kazi hiyo maana bila mkono wa shirika yeye peke yake hataweza.

Naye Mratibu Msaidizi, Mhe. Irene Maganga amemshukuru Jaji Maghimbi  kwa kumteua kuwa Mratibu Msaidizi na kukiri kuwa amefurahi  japo hakuwahi kuwaza lakini ameahidi kumsaidia vema Mratibu Mkuu.

Katika hafla hiyo, kulikuwa na burudani mbalimbali na mashindano ya michezo ya karata, kucheza ngoma kuimba, kuogelea na kombolela ambapo washindi walipewa zawadi.

Hafla waliiita jina la “Sneakers & Jeans Day” ambapo wanachama waliohudhuria walivaa ‘jeans’ na raba.

Wana TAWJA wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla yao iliyofanyika tarehe 01 Mei, 2026 Kigamboni jijini Dar es Salaam.


 Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na Mlezi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Mhe. Salma Maghimbi wakati wa hafla ya Wanachama wa TAWJA Kanda ya Dar es Salaam iliyofanyika tarehe 01 Mei, 2026 Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Wanachama cha Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla iliyowakutanisha Wana-TAWJA Kanda ya Dar es Salaam tarehe 01 Mei, 2026.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam  na Mlezi wa TAWJA  Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi akiwasili kwenye hafla ya Wanachama hao akiwa katika vazi maalum la siku hiyo 'Sneaker' na 'Jeans.' 

Sehemu ya Majaji Wanawake Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambao ni Wanachama wa TAWJA wa Kanda hiyo. Katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Butamo Phillip, kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Monica Otaro na kushoto ni Jaji  wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe.Sharmila Sarwatt kwa pamoja wakiwasili katika eneo la tukio wakiwa katika mavazi rasmi ya siku hiyo.

Baadhi ya Wana TAWJA Mkoa wa Dar es Salaam wakicheza karata. 


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Modesta Opiyo (wa nne kushoto) akiwaongoza wana TAWJA kukata keki wakati wa hafla ya Wana-TAWJA Kanda ya Dar es Salaam iliyofanyika tarehe 01 Mei, 2026 Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kamati ya Maandalizi ya hafla ya TAWJA Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja. Kushoto ni Mhe. Aziza Mbadjo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, katikati ni Mhe. Zenas Tarimo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Ilala na kulia ni Mhe. Scola Odeyo. 

Keki maalum iliyoandaliwa kuashiria upendo.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)

 

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni