Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya.
Mahakama ya Rufani ya Tanzania inatarajia
kuendesha Kikao cha usikilizaji wa mashauri 48 ya rufaa za madai katika Masjala Ndogo ya Mbeya kuanzia
tarehe 18 Juni 2026 hadi tarehe 17 Julai, 2026.
Kikao hicho kitakua na jopo moja la Majaji wa
Mahakama ya Rufani wakiongozwa na Jaji wa Rufaa ya Tanzania Mhe. Winifrida
Beatrice Korosso, Majaji wengine katika jopo hilo ni Jaji wa Mahakama ya Rufani
Mhe. Dkt. Mary Calorine Levira na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Agnes Zephania
Mgeyekwa.
Akiwasilisha taarifa katika kikao kilichofanyika
katika ukumbi wa Mahakama Kuu Mbeya, ambacho ni kikao cha maandalizi (Pre-
Session Meeting), Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Agatha Chugulu
alieleza kuwa Jumla ya mashauri 48 ya Rufaa za madai yamepangwa kusikilizwa
katika Masjala Ndogo ya Mbeya.
Aidha Mhe. Chugulu aliongeza kuwa, katika kuhakikisha ufanisi wa kikao hicho na kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ratiba ya kikao ilitolewa kwa wakati na Hati za kuitwa shaurini za wadaawa kwa ajili ya usikilizwaji wa mashauri zimesambazwa na juhudi za kuwapata wadaawa amabao hawajapatikana zinaendelea.
Naye, Mwenyekiti wa kikao hicho, Jaji wa Rufaa
Mhe. Winifrida Korosso, alihitimisha kwa kuomba ushirikiano baina ya wadau na kusisitiza
kuchunga muda wa kufika mahakamani.
“Lengo letu sote ni kupatikana kwa haki kama
kuna changamoto yoyote wasilisha mapema ili tufikie lengo la kutafuta haki kwa
pamoja ni
matarajio yetu kuwa kutokana na mpango wa kusikiliza mashauri kuandaliwa mapema
pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa kila jalada, kikao hiki kitafikia malengo
yaliyokusudiwa,” alisema Mhe. Korosso.
Kikao
hicho kilihudhuriwa pia na Viongozi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya akiwemo
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, Jaji wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya,
Mhe. Tedy Mlimba, Mawakili na Wadau wengine wa Haki Madai.
Mwenyekiti
jopo Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Winifrida
Beatrice Korosso (kulia), akiongoza kikao hicho, kushoto ni Jaji wa Mahakama ya
Rufani Mhe. Agnes Zephania Mgeyekwa.
Viongozi
wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya waliohudhuria kikao hicho, ni Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (kulia), Jaji wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo (katikati) na Mtendaji wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (kushoto).
Naibu Msajili wa
Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Agatha Chugulu (kushoto) akiwasilisha
taarifa katika kikao hicho na (kulia) ni Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya, Mhe. Tedy Mlimba. Ambaye katika kikao
hicho alikaimu nafasi ya Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.
Sehemu ya Wadau walioshiriki katika kikao hicho hoja mbalimbali kwa makini.
Sehemu ya Wadau walioshiriki katika kikao hicho wakifuatilia kwa makini.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni